Tarehe 5 Februari 2016 ni siku ya furaha kwa wana CCM kote nchini ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi kulitokea baada ya Muungano wa ASP (Afro Shiraz Party)ya Zanzibar na TANU(Tanganyika African National Union) ya Tanganyika.
Tunastahili kuisherehekea siku
hii kwa nderemo na vifijo kwa sababu ya mafanikio
makubwa ambayo Chama chetu kimeendelea kupata ndani na nje ya Chama na katika kuliongoza taifa letu kwa takribani miaka . Katika miaka 39 ya uhai wake Chama chetu kimezidi kuimarika na kimeendelea kuliongoza vyema taifa letu:
Amani, utulivu na Mshikamano ni maendeleo yanayoonekana na yanayosimamiwa na CCM.
Tumeeendelea kuaminiwa na kutumainiwa na Watanzania kama hata mwaka jana ,2015, ilivyojidhihirisha. Kama ilivyothibitika na ushindi wa
kishindo katika chaguzi zote tangu mfumo wa vyama
vingi uanze mwaka 1995 mpaka sasa. Tunazidi kuongoza kwa idadi kubwa ya wenyeviti wa mitaa/vijiji, madiwani, pamoja na wabunge.
Ninaposema hivyo nawaomba wana CCM wenzangu tusibweteke tukadhani kwamba ndiyo tumekwishafika. Bado safari ndiyo kwanza tumeianza
na inaweza kuwa na changamoto zake. Lazima tufanye kazi tena kazi kubwa sana ndipo tutakapojihakikishia
ushindi zaidi kwa chaguzi zitakazoendelea 2019 na 2020. Nguvu ya ushindi inaanzia kwenye Chama. Lazima tuhakikishe tunao umoja wa dhati na kwamba wanachama wetu wanakuwa na mwamko wa hali ya juu wa kukipigania
Chama kwa moyo wetu wote.
Naomba nitangulize pongezi na kuwahakikishia kwamba CCM imewapatia watanzania viongozi bora ambao hawatawapa wananchi mashaka wala kuwa na majuto kwanini waliwachagua. Pongezi zinaenda kwa Rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Joseph Maghufuli kwa kipindi hiki cha siku 60 kuanzia aingie ikulu anatekeleza falsafa ya "Hapa Kazi Tu" vizuri. Tumtie moyo na kumwombea kwa MUNGU ampe usalama na afya tele.
Mafanikio ya miaka 39 ya Chama chetu yasitufanye tubweteke. Bado tunayo kazi kubwa mbele yetu. Ili tuendelee kuongoza dola hatuna budi tuendelee kuwa tumaini na kimbilio la wananchi wetu.
Inatupasa kuwa waaminifu kwa ahadi zetu na watiifu kwa matakwa yao. Kubwa sana, tunatakiwa tuwe tayari wakati wote kubadilika na kwenda na wakati. Tunaweza kufanya
hivyo ikiwa tutaendelea kukuza demokrasia ndani ya chama chetu na kuruhusu na kuvumilia tofauti za mitazamo. Hiyo ndiyo siri ya uhai wa CCM ambayo
hatuna budi kuendeleza.
Kufurahia Sherehe hizi bila kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dr Jakaya Kikwete na timu yake toka mwaka 2007 itakua haina busara.Kwakweli Mwenyekiti wetu ameifanya CCM kuzidi kuwa Imara na yenye nguvu kutoka kwa watangulizi wake. Mafanikio makubwa yaliyoonekana katika kipindi cha Uenyekiti wake ni wakutukuka na kutukuzwa na anastahili pongezi nyingi
Ameifanya CCM kuwa moja na hasa ameifanya CCM kufikika kwa kila mtanzania ndani ya nchi kila kona ya Tanzania.
Pia pongezi ziende kwa Katibu mkuu wa CCM comrade Abdurahaman Kinana na sekretarieti yake yote kwa kuhakikisha Wanamsaidia Mwenyekiti katika kuendeaha shughuli za chama katika umoja na uhodari uliotukuka..bila shaka ile kauli mbiu yetu ya kila siku ya "UMOJA NI USHINDI" imedhihirika kwa vitendo.
Leo ni siku ya furaha kwetu sote. Wakati tukisherehekea mafanikio yetu tuwakumbuke pia waasisi
wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyekuwa mwenyekiti wa TANU na Ndugu Sheikh Aboud Jumbe aliyekuwa Mwenyekiti wa ASP kwa busara, hekima na
uamuzi wao uliotukuka uliowezesha kuzaliwa kwa CCM.
Tunawakumbuka pia wale wote waliotangulia mbele ya haki ambao walijitoa maisha yao kujenga CCM. Hatuna
budi kuwaenzi kwa kutoa mchango mkubwa zaidi mwaka ujao na miaka mingi ijayo. Tuhakikishe kuwa tunaimarisha Chama chetu na kutenda mema kwa ajili ya nchi yetu na watu wake. Hili linawezekana ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake.
Kidumu Chama cha
Mapinduzi!!!!
Sherehe hizi za Chama Cha Mapinduzi zinapambwa na kauli mbiu kabambe ya "Sasa Kazi, Kujenga Nchi na Kujenga Chama"
Hitimisho za Sherehe hizi zinafanyika kitaifa Mkoani Singida tarehe 6 Frbruari ambapo Mwenyekiti wa CCM tqifa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi baada ya sherehe hizi kufunguliwa kule Zanzibar na Makamu mwenyekiti wa CCM zanzibar na Rais wa Zanzibar Dr. Ally Mohamed Shein.
Salima Moshi
Katibu Itikadi Na Uenezi.
No comments:
Post a Comment