ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 1, 2016

SALAMU ZA SHUKRANI.


Kwa niaba ya CCM TAWI LA WASHINGTON DC VIRGINIA NA MARYLAND  Napenda kuwashukuru WaTanzania Wote kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki Mazishi ya mpendwa wetu Baba yetu  Ndugu yetu Mzee George Sebo  Bila kujali Itikadi wala Dini zetu,  hivi ndivyo tulivyo watanzania siku zote, na huu ndio uzalendo. 

Ni dhahiri kuwa tutamkumbuka Mwenyekiti wetu wa CCM daima kwa busara na  hekima zake  zilizotuunganisha pamoja na kuwa kitu kimoja. Hatuwezi kusahau utani wako, ucheshi wako na Upendo wako kwa kila mmoja wetu hapa USA bila kujari itikadi zetu za kisiasa wala kidini. Ni dhahiri umeacha pengo kubwa lisilozibika.

Mwisho kabisa nazidi kuwashukuru kwa mara nyingine tena Watanzania wote, ndugu, jamaa na marafiki kwa Upendo wao.

Ahsanteni.

Imetolewa na:

Salma Moshi

Katibu Mwenezi wa CCM DMV.

01/02/2016

No comments: