Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akieleza maamuzi ya serikali kupeleka chakula cha msaada kwa Waathirika wa maafa ya mafuriko wa kijiji cha Ikwiriri wilayani Rufiji, tarehe 16 Februari, 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa ya mafuriko alipofika wilayani Rufiji kukagua athari za maafa hayo, (wa kwanza kushoto) ni Mbunge wa jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa na Mbunge wa jimbo la Kibiti, Ally Ungwando na kulia kwake ni Mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu, tarehe 16 Februari, 2016.
Mkazi wa kijiji cha Mayuyu wilayani Rufiji, Suleiman Idd akishukuru kwa serikali kuwapatia chakula cha msaada waathirika wa maafa ya mafuriko kijijini humo wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (hayupo pichani), alipofika kijijini humo kukagua athari za maafa hayo tarehe 16 Februari, 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akiangalia sehemu ya njia iliyokuwa ikitumiwa na wananchi wa kijiji cha Utete wilayani Rufiji ambayo kwa sasa wanatumia mitumbwi kuvuka kuelekea kijijini humo kutokana na njia hiyo kufurika maji, wakati akikagua athari za maafa ya mafuriko wilayani humo , tarehe 16 Februari, 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mayuyu wilayani Rufiji wakati alipofika kijijini humo kukagua athari za maafa ya mafuriko tarehe 16 Februari, 2016.
No comments:
Post a Comment