Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho Khalid Ramadhani ‘Tundaman’.
MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho Khalid Ramadhani ‘Tundaman’’ hatimaye amepata dili la ubalozi wa kampeni ya kuhamasisha wanawake wa Africa kuhusiana na tamasha la wanawake liitwalo (AFWAB AMSHA MAMA2016).
Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy na Candy Records,Joe Kariuki.
Tamasha hilo ambalo lilianza tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, kunako Hoteli ya nyota tano ya The Tribe na vitongoji vya Nairobi, Kenya, mfanyabiashara mashuhuri na mwenye jina kubwa music , alifanya bonge la tamasha liliacha gumzo kwa kuvuta maelfu wa watu kutoka kila kona ya dunia. Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy na Candy Records, Joe Kariuki, aliratibu tamasha maridadi lililojulikana kama Amsha Mama, maalum kwa Wanawake wa Kiafrika, tamasha lililofanyika katika Hoteli ya kifahari ya Tribe, sehemu ambayo ni maarufu sana pia kwa wasanii
kutoka Marekani, akiwemo Akon. Tamasha hilo ambalo lengo kubwa lililenga kuzungumzia bayana hali halisi ya maisha ya mwanamke wa Afrika kuhusu safari yake, mapigano yake kimaisha, mafanikio, biashara, ubunifu na ushindi wake katika maisha. Kama mwanaume ambaye siku zote aliye karibu na moyo wa mwanamke ambaye alitaka kumtuza ama kumzawadia kwa hatua aliyofikia, kumtia moyo, kumhamasisha katika safari yake ya mafaniko katika jamii hii yenye mfumo dume barani Afrika. Akizungumza katika event hiyo, Joe alisema: "Kuwawezesha wanawake ni muongozo katika jamii, nami nataka kutumia ujuzi wangu na uzoefu nilionao kujenga jukwaa kwa ajili ya wanawake kukua biashara zao." Washiriki wengi ambao ambao wengi wao walisafirishwa kutoka nchi za mbali kwa ajili ya kuhudhuria ‘event’ hiyo, waliunga mkono mawazo ya Joe, mfano Uganda na Italia. Lisa raia wa Italia alisema: "Dhana ya Amsha Mama ni ya kipekee. Naangalia wanawake wenye uwezo wa kuzalisha hila zitakazotumika huko Milan. " Sophie kutoka Uganda, alisema: "Ninawezaje ku-miss hii! Kama mwenyekiti wa chama chetu cha wanawake 600 nataka kuhakikisha wanapata aina hii ya fursa kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zao na kwa ajili ya kupata mtandao na wanawake wengine." Rundo la wanawake waliokuwa na hisia kama hizo, akiwemo mwingine kutoka Copenhagen, Denmark: "Tamasha haya ndiyo tunahitaji kwa ajili ya kukuza wanawake. Inaonyesha nguvu za wanawake na mipango yao." Na katika hilo, Joe anaendeleza jitihada zake za si tu kumwezesha Mwanamke wa Afrika, bali pia kumuinua, kumtia moyo wake, kumpa mwangaza na kujihusisha kwake. Hivyokwa sasa na ndiyo maana ameandaa maonyeshwa makubwa ya wanawake (AFWAB AMSHA MAMA 2016), yatakayofanyikia katika Uwanja wa Kedong ranch uliopo katika jiji la Naivasha nchini Kenya Machi 25-27 2016.
No comments:
Post a Comment