ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 23, 2016

VODACOM TANZANIA KUPITIA PROGRAMU YA PAMOJA NA VODACOM WATOA MSAADA WA MASHINE YA KUDURUSU KARATASI SHULE YA SEKONDARI SHIMBWE.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini,Jacob Costantine akimueleza jambo Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaksakazini,Henry Tzamburakis alipofika shuleni hapo kwa ajili kukabidhi mashine ya kisasa ya kuduru karatasi.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom imekabidhi kwa shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilaya ya Moshi vijijini ,msaada wa mashine yenye uwezo wa kufanya kazi zaidi ya tatu ikiwemo kudurusu karatasi.


Msaada wa mashine hiyo (Photocopier) yenye thamani ya zaidi ya sh Mil 12 ni sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo kampuni hiyo kupitia mradi wa “Pamoja na Vodacom” imekabidhi shuleni hapo zikiwemo Kompyuta mpakato 30.


Mbali na msaada wa Kompyuta na Mashine hiyo kampuni hiyo pia ilitoa wataalamu kutoka shirika lisilo la kiserikali la Learning  in Sync kwa ajili ya kuweka program maalumu katika kmpyuta za kufundishia na kujifunzia .


Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis alisema kutolewa kwa mashine hiyo ni muendelezo wa msaada ambao Vodacom kupittia mradi wa Pamoja na Vodacom imeendelea kutoa kwa nchi nzima.


“Huu ni muendelezo wa msaada ulitolewa awali ,Kampuni ya Vodacom tunarudisha sehemu ya faida kwa wananchi na wateja wetu,pamoja na hayo ni kusaidia wadogo zetu kuingia katika digitali wakiwa na umri mdogo na kuwaandaa na maisha ya baadae,”alisema Tzamburakis.


Alisema Mashine hiyo ya kisasa itasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo hususani katika maandalizi ya mitihani pamoja na machapisho mengine ambayo shule ili lazimika kuingia gharama kubwa kuchapisha.


Katika kuhakikisha walimu wa shule hiyo wanaweza kutumia vyema mashine hiyo Tzamburakis alisema ofisi ya Vodacom kanda ya Kaskazini itatoa mtaalamu kwa ajili ya kufundisha namna ya kuitumia.


“Ofisi ya kanda ya Vodacom ina wataalamu wa IT ambao watasaidia katika kutoa mafunzo kwa walimu ya namna ya kutumia mashine hizi na tutaweka utaratibu wa kufika mara moja kwa mwezi katika shule hii ili waweze kubadilishana uzoefu na walimu wa masomo hayo.”alisema Tzamburakis.


Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa msaada huo huku akieleza changamoto zilizoikabili shule hiyo ikiwemo ya kuchapisha mitihani kwa gharama kubwa .


“Tumepewa mashine ya Photocopy ikiwa ni ahadi ya mgeni rasmi kutoka Vodacom baada ya kumueleza kuwa tumekuwa tukitumia gharama kubwa hasa kipindi cha mitihani ,kuchapisha mitihani yetu ya mihula na ile ya mwisho wa mwaka”alisema Costantine.


Alisema kupatikana kwa mashine hiyo ,sasa shule itakuwa na uwezo mkubwa wa kuchapisha machapisho mbalimbali vikiwemo vitabu ambavyo upatikanaji wake umekuwa mgumu kwa ajili ya wanafunzi hao kujifunzia.


Mkuu huyo wa shule alisema wamekuwa wakitumia zaidi ya shilingi Milioni nne kwa ajili ya maandalizi ya mitihani shulebi hapo na kwamba kwa sasa adha ya kuandika ubaoni mitihani ya majaribio itatoweka.


Mwisho.

No comments: