Watu saba wameuwawa kwa kupigwa
risasu akiwemo mtoto wa miaka nane huku wengine kadhaa wakijeruhiwa
katika tukio la mauaji lililotokea huko Kalamazoo, Michigan nchini
Marekani jana usiku.
Mkuu wa Usalama wa Umma wa Kalamazoo
Jeff Hadley mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa leo asubuhi.
Polisi wamesema mtuhumiwa huyo
amekamatwa kwenye gari linaloshabihiana na lililotumiwa mshambuliaji,
ambapo pia bunduki ilipatikana kwenye gari hilo.
Mtuhumiwa huyo mzungu mwanaume
mwenye umri wa miaka 45, ni mkazi wa kaunti ya Kalamazoo, imeelezwa
alijisalimisha bila ya purukushani.
No comments:
Post a Comment