Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Magereza nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Magereza nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wapili upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Wapili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja akifuatiwa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi hilo, Dk. Juma Malewa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja (kushoto) akijitambulisha kabla ya kuanza kikao cha Watendaji Wakuu wa Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kilichoitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment