Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma unaojulikana kwa jina la Public Sector Systems Strenghening (PS3) unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla. Mkutano wa uzinduzi huo utakaofanyika kwa siku mbili Machi 09,2016 hadi Machi 10,2016 umehudhuriwa na Kiongozi wa timu ya mradi,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,wataalam kutoka kutoka ofisi ya Waziri mkuu na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi,mashirika na taasisi za umma na binafsi-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yupo eneo la tukio ametusogezea picha 30 ,Tazama hapa chini
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla. Mkutano wa uzinduzi huo utakaofanyika kwa siku mbili Machi 09,2016 hadi Machi 10,2016 umehudhuriwa na Kiongozi wa timu ya mradi,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,wataalam kutoka kutoka ofisi ya Waziri mkuu na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi,mashirika na taasisi za umma na binafsi-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yupo eneo la tukio ametusogezea picha 30 ,Tazama hapa chini
Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ambaye pia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Public Sector Systems Strenghening(PS3) utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano na utafanya kazi na serikali kuu pamoja na halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
Wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini,wa kwanza kushoto ni Vita Kawawa kutoka wilaya ya Kahama,akifuatiwa na Josephine Matiro kutoka wilaya ya Shinyanga na Hawa Ng'umbi kutoka wilaya ya Kishapu
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua mradi wa PS3 ambapo alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 13 nchini ambayo itanufaika na mradi huo ambapo alidai umeanza kwa wakati muafaka kwani sasa serikali iliyopo madarakani inataka mabadiliko katika kuhakikisha kuwa serikali inahudumia wananchi ipasavyo
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) akifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Rufunga alisema mradi huo utakuwa na tija kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliwataka watendaji wa serikali katika ngazi ya mkoa na mamlaka za serikali za mitaa kutoa ushirikiano katika kutekeleza mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma kutokana na kwamba wao ndiyo wana mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi wa kawaida.
Tunamsikiliza mgeni rasmi......
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)
Meneja wa Mradi wa PS3 Dkt Emmanuel Malangalila akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo ambapo alisema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano umeandaliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na kutekelezwa na mashirika saba likiwemo shirika la Abt Associates Inc ambalo ndiyo mtekelezaji mkuu.
Dkt Malangalila alisema mradi huo utasaidia uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya mamlaka za serikali za mitaa ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi,kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga,kufuatilia na kutoa matokeo katika kila sekta.
Dkt Malangalila alisema,PS3 pia itasaidia katika kuongeza pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma,usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora na kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa na kuwepo kwa tafiti tendaji kusaidia mradi ili kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo.
Mratibu wa mradi wa PS3 kutoka ofisi ya Waziri mkuu TAMISEMI Beatha Swayi akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo alisema mradi huo utatekelezwa katika halmashauri za wilaya kwenye mikoa 13 nchini na mkoa wa Shinyanga umekuwa wa pili kuzindua mradi huo baada ya katika mkoa wa Iringa kuzindua mradi huo mwezi Februari Mwaka huu.
Swayi alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa serikali katika halmashauri kuwajibika ipasavyo ili kufanikisha mradi huo uliojikita katika kuboresha utumishi wa sekta za umma.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 ambapo aliwashukuru wafadhili wa mradi huo kwa kuona umuhimu wa kuufikia mkoa wa Shinyanga
Uzinduzi unaendelea
Uzinduzi unaendelea....
Uzinduzi unaendelea
Kulia ni Meneja wa Mradi huo Dkt Emmanuel Malangalila akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Mtakwimu ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo alisema mradi wa PS3 umeandaliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na kutekelezwa na mashirika saba ambayo ni Abt Associates Inc kama mtekelezaji mkuu na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa(BMF)
Dkt Malangalila alisema watekelezaji wengine wasaidizi wa mradi wa PS3 ni Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM),Chuo cha Mafunzo ya serikali za mitaa Hombolo(LGTI),Taasisi ya Ushauri Tanzania(TMA)Broad Branch Institute,Intra Health International na Urban Institute.
Waandishi wa habari wakiwajibika.
Dkt Malangalila alisema mikoa itakayonufaika na mradi huo kuwa ni Shinyanga yenye halmashauri za wilaya sita na Iringa.
Mikoa mingine ni Dodoma,Kagera,Kigoma,Lindi,Mara,Mbeya,Morogoro,Mtwara,Mwanza,Njombe na Rukwa.
Kiongozi wa Utawala bora na Ushirikishwaji wa raia katika mradi wa PS3 Dkt Peter Kilima akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari,ambapo aliviomba vyombo vya habari kushiri kikamilifu katika kutekeleza mradi huo
Kushoto ni mratibu wa mradi wa PS3 mkoa wa Shinyanga Mohamed Marais akieleza namna mkoa wa Shinyanga ulivyojipanga kutekeleza mradi huo
Picha ya pamoja mgeni rasmi Ally Nassoro Rufunga,meneja wa mradi wa PS3,mratibu wa PS3 kutoka ofisi ya waziri mkuu,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya ,meya wa manispaa ya Shinyanga na wenyeviti wa halmashauri za wilaya katika mkoa wa Shinyanga
Picha ya pamoja mgeni rasmi Ally Nassoro Rufunga,meneja wa mradi wa PS3,mratibu wa PS3 kutoka ofisi ya waziri mkuu,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya ,meya wa manispaa ya Shinyanga na wenyeviti wa halmashauri za wilaya katika mkoa wa Shinyanga
Picha za pamoja zikaendelea kupigwa
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
No comments:
Post a Comment