ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 22, 2016

CCM DMV MAREKANI PONGEZI ZA USHINDI MKUBWA


TUNATOA PONGEZI ZETU ZA DHATI KABISA KWA MH RAIS MTEULE DR ALI MOHAMEDI SHEIN KWA USHINDI MKUBWA ALIOUPATA KWENYE UCHAGUZI TUNATOA PONGEZI KWA WANANCHI WA ZANZIBAR KWA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI KUMCHAGUA DR SHEIN AWE RAIS NA CCM KUENDELEA KUONGOZA HII INAONYESHA IMANI KUBWA MLIYOKUWA NAYO KWA CCM SASA WOTE TUWE WAMOJA NA MSHIKAMANO UMOJA NA AMANI HONGERA SANA MH. SHEIN NA WANANCHI ZANZIIBAR.

SALMA MOSHI. 

KATIBU ITIKADI NA UENEZI. 

CCM DMV MAREKANI.

7 comments:

Anonymous said...

REALLY?

Anonymous said...

Salma. Nilidhani ungetafakari kwanza hali halisia kumbe na wewe uummoja waudhalimu! Kuna ukweli gani hapo na uhakika gani wa haki kutendeka ni waZanzibari, waUnguja wangapinwalopiga kura. Usituingize huko wengine kwa kusema DMV?! Hayo ni mawazo yako mwenyewe hayatuhusu. Zanzibar inaongozwa kimtindo wa kulazimisha. Ni mwana CCM lakini kwa hilo vyema tuwe wakweli tu! Asilimia??? Ya aina gani hiyo! Kasherehekee nao nyumbani ingekuwa bora mdogo wangu!,

Anonymous said...

Asante. Salma ila kwa mtizamo wangu hii siyo kauli ya wana DMV umeipachikia kama alivyopachikwa unayemsifia! Huyu mheshimiwa amewekwa pale bila ridhaa ya wananchinwa Zanzibar na ninkimyume na taratibu za nchi!? Hatuhitaji kulumbana huo ndio ukweli usiofichika.

Anonymous said...

Kuweni na utuuu.unajua fika dhulma inetendeka halafu unashangiti.. Uneambiwa katikadini japo chukia tuu ndani ya moyo kama unashindwa kuondoa dhulma.. Usijiinginr kwenye maangamizo ambayi ushapewa fursa ya japo kuchukua ingawa ni udhaifu wa iman..Zanzibar hakuna raisi halali ya ridhaa za wazanzibari pale.. Ni watu kuweka mbele dunia wakasahau akhera yao.mungu tuongoe kwa sote na umpe ujuzi mwenye kudhulum ili atambue na awache hilo.. Ameena

Anonymous said...

Ndio kasha kaa yaheee mnaumiza kichwa wakati maalimu sharifu anawasaliti cuf kimtindo

Anonymous said...

Salma, lazima ifike Wakati uwe unafikiria kabla ya kuandika. Kwa Lugha ya mtaani ni kuwa, unapayuka Zaidi ya kujenga hoja. Mwisho unashabikia kunyimwa uhuru WA Wazazibari kutoka mikononi mwa wakoloni WA Tanganyika kupitia CCM. Wazanzibari, fanyeni kama walivyofanya Eritrea kuingia msituni kupambana na ukoloni, huu sasa siyo WA wazungu Bali wa weusi toka Tanganyika.

Anonymous said...

Wewebabu sheni wewe ona aibu.. Umegeuka pweza una jikusanyia mkaa wa moto.. Hutuba ya nini wakati sio raisi wewe. Muogope mungu.. Uhai wa miaka 63 usikubabaishe ukawacha akhera yako...