Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimpatia hati ya kiwanja cha Vikuruti, mteja wao Ibrahim Yusuph Ismail, nyumbani kwao Kariakoo jijini Dar es Salaam, leo mchana. Kwa wiki hii tu Bayport imeamua kuwapelekea hati za viwanja wateja wao katika maeneo yao ya makazi na maofisini kwao.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabiti Mndeme, kushoto akizungumza jambo wakati anamkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao Neema Jameson Nawita, jijini Dar es Salaam leo mchana.
Na Mwandishi Wetu, Dar esSalaam
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wateja wa Bayport
waliojipatia viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha
mkoani Pwani wameendelea kupewa hati zao, huku safari hii wakipewa hati kwenye
maeneo wanayopatikana ikiwamo majumbani na maofisini. Hatua za kuwapelekea hati hizo wateja wao ni kitendo cha
kuthamini uwapo wa wateja wao wanaoendelea kuiamini Bayport Financial Services
katika bidhaa zake za mikopo ya fedha, bila kusahau huduma ya mikopo ya viwanja
vyenye hati inayotolewa na taasisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau wa ardhi
walioingia mikataba na Halmashauri unapopatikana mradi wa viwanja kwa ajili ya
watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi, wajasiriamali na Watanzania
kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa kutoa hati kwa wateja watatu leo jijini Dares Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema jambo kubwa la miradi ya viwanja kwenye taasisi yao ni kuona weteja wao wanapata hati ili kuweka ubora wa huduma zao, ikiwa ni sehemu muafaka ya kufuta migogoro ya ardhi kwa kununua viwanja vyenye hati. Alisema kwa wiki mbili mfululizo wamekuwa wakiendelea kutoa hati kwa wateja wao, huku kwa wiki hii tu, taasisi hiyo ikifika mbali kwa kujenga imani na kwenda sambamba na wateja hao, wakaona umuhimu wa kuwathamini na kuwataka wachague maeneo wanayoona wanaweza kupokea hati zao, iwe ni maofisini kwao au kwenye maeneo ya makazi.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita, kulia akipokea hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, aliyokabidhiwa leo na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita,kulia akizungumza na waandishi baada ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi,wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kushoto ni Thabit Mndeme, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani mteja wao Hassan Omary Hamis, jijini Dar es Salaam, leo mchana.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhi hati ya kiwanja kwa Hassan Omary Hamis
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akizungumza jambo wakati anakabidhi hati za viwanja kwa wateja wao wa Bayport Financial Services hawapo pichani leo jijini Dar es Salam.
“Huu ni utaratibu tulioamua kwa wiki mbili hizi kwa wateja waliokuwa wanapokea hati tuwafikishie kwenye maeneo yao ili waone taasisi yetu inawathamini na kuwashukuru kwa sababu wamekuwa wakiendelea kuunga mkono bidhaa zetu zote, ikiwamo huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti tulivyoanzisha mwaka jana na mwaka huu tukianzisha huduma za viwanja katika maeneo ya Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kilwa na Kigamboni. “Huduma hizi ni nzuri kwa Watanzania wote mahala popote walipokuwa wanaweza kukopa au kununua viwanja hivi kwa njia pia ya fedha taslimu, ambapo kwa (Kimara Ng’ombe) Bagamoyo mita moja ya mraba inauzwa Sh 10,000, (Msakasa) Kilwa Sh 2000, (Boko Timiza) Kibaha Sh 9000, (Tundi Songani) Kigamboni Sh 10,000 na (Kibiki na Mpera) Sh 4500, ambapo huduma zetu zinapatikana pia kwenye matawi yote yaliyoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara,” Alisema Mndeme.
Naye Neema Jameson Nawita aliwashukuru Bayport kwa kumpatia hati yake bila usumbufu wowote, akisema huduma zao za viwanja zinaonekana kuandaliwa vyema huku zikiwa hazina usumbufu wowote katika kuandikishwa hadi upewaji wa hati zao. “Nimefurahi kwa sababu nimefanikiwa kuwa miongoni mwa Watanzania waliopewa hati za viwanja vya Vikuruti baada ya kununua kiwanja hicho mwaka jana na nzuri zaidi nimepata bahati kubwa kwa sababu nimeletewa hati hadi eneo la ofisi yangu,” Alisema.
Naye mjasiriamali Ibrahim Yusuph Ismail aliipokea hati yake shangwe na kusema kufanikiwa kununua kiwanja cha Vikuruti na kupewa hati yake bila usumbufu ni hatua nzuri na mwendelezo wa kujiendeleza kwa kutumia rasilimali bora ya ardhi.
Mteja mwingine aliyezungumzia hatua hiyo ya upewaji hati ni Hassan Omary Hamis, ambaye aliwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa bora ya uwekezaji wa ardhi kwa kujenga nyumba za makazi na za biashara ili waongeze wigo wa kipato chao.
“Tusiogope kuwekeza kwa sababu ni jambo la msingi ukizingatia kwamba zipo taasisi zenye kiu ya maendeleo wakiwamo Bayport, maana si lazima mtu anunue kwa pesa taslimu, ila anaweza kununua kiwanja kwa njia ya mkopo usiokuwa na usumbufu na ukiwahusu watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali,” Alisema.
No comments:
Post a Comment