Ndugu zangu,
Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa. Nikasema Edwad Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.
Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.
Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.
Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.
Naomba radhi kwa familia ya baba wa taifa mwalim Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.
Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata nyerere mpya.
Mungu Ibariki Tanzania
mungu Ibariki Afrika
Balozi Juma Mwapachu
2 comments:
Hatuna haja nawe mzee. Nenda kamsaidie Lowasa kuchunga ng'ombe zake. Uliondoka ili kutuletea balaa tushindwe uchaguzi na sasa unataka kurudi ili kutuletea balaa tusiweze kuijenga nchi yetu? Hapa Kazi tuu, CCM itaendelea kuwika bila nyie ndumakuwili.
YALE YALE. HII NI WAZI KUWA HUYU MTU NI MBINAFSI. HATA HIVYO UBINAFSI UNABAKI KUWA NI TABIA YA MTU BINAFIS. LAKINI, TATIZO NI PALE MTU KAMA MWAPACHU ANAPOENDEKEZA UBINAFSI WAKE KWA KUTOA KAFARA WATANZANIA, INASIKITISHA SANA! SINA TATIZO NA KAMWE SITAKUWA NA TATIZO IWAPO MWAPACHU ANGEITOA KAFARA FAMILIA YAKE, LAKINI HILI LA KUWAHADAA WATANZANIA NI AIBU NA INASIKITISHA!
Post a Comment