Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini Mwanza kushiriki zoezi la utoaji wa msaada wa vifaa mbalimbali kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza. (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali, Chama pomaja na Wananchi walifika kumpokea alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika Kituo cha kulea
wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza wakati wa hafla ya
kutoa msaada wa vifaa mbalimbali na kuyashukuru mashirika, Taasisi za
serikali pamoja na sekta binafsi kwa kutoa misaada hiyo ikiwemo Mchele,
Unga, Maharage, Mafuta ya kupikia, mashine za kufulia pamoja na solar
panel pia akatoa rai kwa wadau wengine kujitolea kusaidia wazee na watu
wasiojiweza.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akimkaribisha Mama Janeth Magufuli
kuongea na Wazee na pia kuwahakikishia wazee kuwa serikali ya awamu ya
tano itaendelea kusimamia katika ahadi zake hasa katika kuhakikisha
wazee wanapata huduma bila usumbufu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali, Chama pomaja na Wananchi walifika kumpokea alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiangalia burudani ya ngoma alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
Baadhi ya misaada iliyotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shada la maua alipowasili kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa heshima na kuwasalimia wananchi walifika kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei.
Baadhi ya sehemu ya wazee wakiimba kwa furaha wakati hafla ya utoaji wa Msaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mwajuma Nyiruka akiongea na wananchi waliojitokeza katika hafla ya utoaji wa Msaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza na kumshuruku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa kushiriki katika hafla hiyo.
Afisa Mfawidhi na Mlezi wa Kituo kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza kilicho chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii Bw. Michael Bundala akiongea na wananchi na kushukuru wadau waliotoa msaada katika kituo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akiongea na wazee wa kituo kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza, wananchi waliohudhuria hafla ya utoaji wa Msaada katika kituo hicho na kumshukuru Mama Janeth Magufuli kwa kuwakumbusha juu ya utoaji msaada na kuwajali wazee na watu wasiojiweza na kumahidi kuandaa sera mpya ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma na wazee wa Kituo kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kumaliza kuongea na wazee
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kumaliza kuongea na wazee
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akishiriki katika kukabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo CRDB, PPF na Makampuni binafsi kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akishiriki katika kukabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo CRDB, PPF na Makampuni binafsi kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee katika kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na watoto wakati wa hafla ya utoaji wa Misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza Bukumbi Mkoani Mwanza
No comments:
Post a Comment