ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 28, 2016

MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 ZINAFANYIKA JUMAPILI HII VIWANJA VYA KIA,KILIMANJARO.

Mratibu wa Mashindano ya Mbio za Magari ya Vaisakh Rally 2016 ,Faheem Aloo akiwa na Mwenyekiti wa matukio wa klabu ya Kilimanjaro Motorspot ,Juma Shaaban.
Mratibu wa Mashindano ya Mbio za Magari ya Vaisakh Rally 2016 ,Faheem Alooakizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani ) kuhusu maandalizi ya Mbio za Vaisakh Rally 2016 zinazofanyika Jumapili hii katika viwanja vya KIA.

Mkuu wa Usalama wa Kampuni ya Security Group (SGA) Absolom Jailo akizungumza namna ambavyo kampuni hiyo imejipanga kuimarisha ulinzi katika mshindano hayo.
Mkuu wa Huduma ya Kwanza katika mashindano hayo Dkt Akshay Prataap akieleza namna walivyojipanga kutoa huduma ya kwanza endapo kutatokea tatizo kwa madereva wanaoshiriki mbio hizo.
Zawadi kwa washindi.
Hari Singh Rally Team ni moja ya madereva walioingiza gari mpya aina ya Subaru za mwaka 2015 katika mashindano hayo.
Jamil Khan ataongoza team Evolution katika mashindano hayo.
Raia wa Italiano Piero Canobbio ni mmoja wa madereva ambao wanatajwa kuwa tishio katika mbio hizo ambaye anashiriki kwa mara ya kwanza akitokea nchini Kenya.
Magari ya Mashindano yakijipanga kwa ajili ya ukaguzi wa mwisho .
Gurjit Dhan Dereva anayepewa nafasi kubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.
Dereva Larry Horn anaingia katika mashindano hayo akiwa na gari aina ya Porche.
Baadhi ya magari yanayoshiriki mashindano hayo yanayofanyika Jumapili hii katika viwanja vya KIA,

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: