Ungana na Wanahabari kupaza sauti kurejeshwa kwa Mwandishi wa DW na Gazeti la Mwananchi Bi. Salma Saidi..aliyetekwa na watu wasiojulikana na kuwekwa kizuizini nchini Tanzania
Kumekuwapo na taarifa zinazoripotiwa kwa vyombo vya habari za kuhusu kutekwa kwa mwandishi wa habari wa Sauti ya Ujerumani Zanzibar (DW), ambaye pia ni mwanahabari wa gazeti la Mwananchi la hapa Tanzania, Bi. Salma Said (pichani) ambaye ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao hawajafahamika jijini Dar es salaam. Tunaamini hali hii si nzuri kwa mwanahabri mwenzetu na inaleta machungu na fadhaa na mshtuko kwa waandishi, jamii na familia yake kwa kipindi hichi kigumu.
Mtandao huu wa Modewjiblog unaungana na Wanahabari wote kokote pale walipo na familia ya Bi. Salma kuweza kupaza sauti ili mwenzetu aweze kupatikana ama kuachiriwa huru.
Hatuamini watu hao waliomteka mwanahabari kuwa wana nia gani ila, tunaomba kwa Idara husika ikiwemo Serikali ambayo inajukumu la kulinda raia na mali zake kulifanyia kazi suala hili bila kuingilia utaratibu mwingine.
BRING BACK OUR SALMA SAID
BRING BACK OUR SALMA
BRING BACK OUR SALMA
TUNAOMBWA KUACHIRIWA HURU KWA MWANAHABARI SALMA SAIDI.
Ukiwa mwanahabari, Mwanajamii na mtanzania mpenda Amani, ungana katika kupaza sauti ya kurejeshwa kwa Mwanahabari Salma Saidi! Kupitia mitandao ya kijamii na njia nyingine yoyote ile ilikusikika kwa sauti yako.
1 comment:
Tuwe waangalifu na suala hili hasa ukichukulia taimingi ya hii sinema ilivyotokea na inavyoendelea ikiendana sambamba na marudio ya uchunguzi Zanzibar. Nitatoa mifano kama ifuatavyo:-
(1)CUF inawezekana ni muhusika mkuu wa huu unaodiwa utekekajwi nyara wa huyo mama na sababu kubwa iliopelekea kufanyika kwa mpango huo ni kuitia doa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar katika jumuia za ndani na za kimataifa ambao wao wenyewe wameususia.
(1)Mwanadada mwenyewe inawezekana kabisa anahusika na huo unaoitwa utekaji nyara feki kwa maana yakwamba ni mwanahararkati wa CUF na kwa kutumia taaluma ama umaarufu wake kama mwandishi wa habari imeonekana tukio likitokea kwake litakuwa na mvuto zaidi au drawing more attention in a maximum level katika jamii.
(3) Sio mara ya kwanza kutokea kwa matokeo feki ya utekaji nyara na wahusika kuvisingizia vyombo vya dola. Mfano mzuri ile filamu ya kiongozi wa mwamsho Zanzibar alieamua kujiteka nyara ili wafuasi wake washikwe na ghadhabu na kuanzisha mapambano na Serikali na baadhi ya watu walilaumu na kuilani serikali ya mapinduzi Zanzibar kamamba ilihusika kama hivi watu wanavyofanya sasa kwa tokeo la huyu dada lakini mwisho ya siku ikabainika kiongozi huyo wa mwisho alijiteka nyara yeye mwenyewe binafsi.
(4) Wahusika wa tokeo hili la utekaji nyara wameliandaa hili tukio ili kuidhihirishia jumuia za kimataifa na za ndani kwamba uchunguzi wa marudio Zanzibar si wahuru na umejaa vitendo vya kigaidi kwa hivyo matokeo yake si halali.
(5)kama serikali na vyombo vyake vya usalama kama vimehusika katika tukio hili itakuwa sio sahihi hata kidogo na inapaswa kuwajibika, lakini kwa uzowefu wa siasa za CUF na mwamsho Zanzibar kuna asilimia ndogo sana ya serikali kuhusika na hili. Itakuwa ni filamu ya CUF na washirika wake.
(6)Serikali ama ya muungano au ya mapinduzi Zanzibar haina haja ya kumteka mtu nyara kwa mpango gani hasa? Ikiogope nini kumkamata mtu laivu au kumwita kituo cha polisi kwa mahojiano hadi ipelekee kumteka nyara raia wake? Sioni tishio la aina yeyote ile kwa serikali zote mbili kutoka kwa huyu mama hadi wamteke nyara kwa mantiki gani hasa it real doesn't make any sense isipokuwa nia ni kuipaka matope Tanzania serikali yake kwa wananchi wake na jamii za kimataifa kwa wale wahusika waliloliandaa hili tukio.
Post a Comment