Saturday, March 5, 2016

SHAMBA LA KITULO LATUA MIKONONI MWA MWIGULU NCHEMBA,SASA LINAKWENDA KUWA MFANO BARANI AFRICA

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Makete Mh.Noramn Sigalla wakati alipowasili kwenye shamba la Kitulo ambalo ni moja ya Mashamba makubwa ya kufuga Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba.Huwa ni mfano wa Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba wanaopatikana shamba la kitulo wenye uwezo wa kutoa maziwa lita 15 hadi 20 wanapokamuliwa mara moja kwa kila mmoja.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kutoka kwa meneja wa shamba la kitulo kuhusiana na uzalishaji wa Ng'ombe aina ya mitamba.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Makete Ndg.Mh.Mwigulu Nchemba akiwa kwenye shamba la kitulo akipewa maelezo mbalimbali yanayohusiana na kuyumba kwa ufugaji wa ng'ombe kwenye shamba hilo.Moja ya Farasi ambaye anafugwa kwenye shamba la Kitulo,Idadi ya Farasi wanaofugwa imepungua kutokana na wengi kuuzwa kwa wananchi.Moja ya Dume la Ng'ombe la kisasa ambalo limezalishwa Shamba la kitulo.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia namna ukamuaji wa maziwa unavyofanyika kwenye shamba la kitulo.Akiwa njiani kutokea shamba la Kitulo,Mh.Mwigulu Nchemba alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa kata ya kikondo ambao walikuwa na malalamiko ya kulipwa fidia baada ya kuhamishwa kutoka hifadhi ya Kitulo,Madai yao ya fidia ni fedha ya Tanzania Bilion 1.8,Mwigulu amewaahidi kuwasaidia wananchi hao kwa kuzungumza na waziri wa Mali asili na Utalii aweze kuprocess malipo hayo.Mbunge wa Makete,Dr.Norman Sigalla akiomba kwa Waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi kufanikisha zoezi la kuboresha shamba la kitulo ili uchumi wa wananchi wake wa Makete na wanaozunguka shamba hilo uimarike.
Shamba la Kitulo la Ufugaji wa Ng'ombe aina ya Mitamba lilianzishwa mwaka 1963 na Mwl.Nyerere kama eneo la kuzalisha maziwa ya kusambaza nchi nzima,Ng'ombe aina ya Mitamba wanaopatikana kwenye shamba hilo waliingizwa nchini kutokea Marekani na nchi za Ulaya Mashariki ambazo hali yake ya hewa inaendana na ile ya kitulo ambayo kuna wakati ni 0 centgrade,na hali ya juu zaidi inaweza kuwa 19 Centgrade.
Kuanzia miaka hiyo ,Shamba la kitulo ambalo linauwezo wa kulisha ng'ombe elfu nne (4000),Shamba hilo kwa sasa lina ng"ombe mia saba tu(700).
Mbali zaidi,nyenzo za kutunzia ndama na kukamua maziwa haziridhishi na ukuziaji wa nyasi zilizopandwa kwaajili ya malisho haulidhishi.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya kusikiliza na kuona changamoto zinazolikabili shamba la kitulo kwa ufugaji wa ng'ombe,Ameahidi kuhakikisha analiboresha na kusaidia upatikanaji wa ng'ombe wa kutosha,huduma za kutosha ili eneo la kitulo liwe ni shamba darasa hata kwa mashamba mengine ndani na nje ya nchi yetu.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

1 comment:

Anonymous said...

Yaani utaona kabisa kwamba watanzania tunahitaji mikakati au sijui nisemeje? Bidhaa za organics ndio habari ya mjini duniani kote kwa sasa. Nchi kama marekani n'gombe anaelishwa majani kama hao wa kwetu maziwa yake kuyanunua kwa mtu wa kawaida unatakiwa uwe na moyo kutokana na bei yake kuwa juu. Soko la bidhaa za Organics kwa nchi zilizoendelea ni kubwa na lina njaa ya bidhaa hizo wakati Africa ikiwemo Tanzania nnaimani bado tunauwezo makubwa wa kuzalisha bidhaa hizo kwa gharama nafuu na kujipatia kipato kikubwa zaidi kama tutafanikiwa kupata masoko ya nje. Sasa si elewi kwa nchi zetu tatizo liko wapi na kwanini mpaka leo mkulima awe mtu mnyonge na kilimo chetu bado ni duni? Kitu kimoja naweza kusema kwa kinywa kipana, kwa kweli hatupo serious . Niseme wizara nyingi katika serikali zetu zilizopita zilikuwa na watu wa hovyo wa kuziongoza wasio kuwa na mikakati na malengo yanayolenga mbele. Kwa mfano kwanini sekta binafsi kama kina Baharesa zinafanya vizuri hata katika maeneo ya kilimo serikali au mashirika ya kiserikali yashindwe ? Kwa bahati mbaya zaidi hata wale raia wa kawaida waliotegemea kuwezeshwa na mashirika hayo ya kiserikali wamejikuta wakihangaika kwani wataezeshwa vipi wakati hayo mashirika yenyewe ni mashirika yaliofeli, wao wenyewe hawajiwezi. Kwa bahati nzuri nilijaribu kilimo na nilipo jaribu sikutaka kufanya mzaha niliamua na kujituma na kuekeza akiba yangu 75% ya pesa niliokuwa nao wakati huo na haikuwa hela nyingi ila plus my own labor ilikuwa ya nguvu kuliko hata hiyo hela kwa kweli kikanitoa msimu mmoja tu kilimo kikaniondosha Africa na malengo ni kurudia tena huko katika kilimo. Mimi nnaimani kabisa sekta mbili tu za kiuchumi kama nchi yetu itakuw serious nazo, basi hatuhitaji hata kuhangaika katika uvumbuzi wa mafuta. Sekta hizo ni kilimo na utalii. Katika upande wa biashara ya utalii matatizo yake sawa sawa na yale kwenye kilimo. Kuna mahotel makubwa ya kitalii yaliojengwa na serikali yamefeli na mengine kufikiwa kuuzwa, kwanini biashara ya hotel ifeli? Nnaimani kabisa kama kulikuwa na Kilimanjaro hotel moja daresalam tangu wakati huo sasa hivi ilistahili kuwa ilishatengeneza chain of Kilimanjaro hotels karibu ukanda mzima wa east Africa au Africa nzima kwa ujumla,hivyo ndivyo wenzetu wanavyofanya biashara siku zote kwa biashara kuja kujidhalisha na kujiendesha wenyewe . Ukienda pale Miami Florida utaikuta the first Sheraton Hotel of the Sheraton chain Hotels. Sasa Sheraton Hotel ni dunia zima. Russia kahitalifiana kibiashara na karibu na nchi nyingi za ulaya. Kasusia bidhaa zao baada watu wa ulaya kushawishia na mmarekani wamwekee vikwazo. Soko la Russia ni kubwa mno kupita kiasi kiutalii na bidhaa za kilimo kwa kweli ilikuwa ni Golden opportunity kwa nchi zetu kumuhakikishia usalama wa mahitaji yake wa bidhaa anazohitaji zipo chini himaya yetu na asahau bidhaa za ulaya. Wale watu wa ulaya wana miezi minne ya kilimo ikizidi sana sita kutokana na hali ya hewa yao lakini wanatoa misaada chakula kwa nchi za Africa zenye hali ya hewa inayoruhusu uzalishaji karibu mwaka wote? Sasa nchi zetu zingekuwa na uwezo kumtosheleza angalau robo ya mahitaji yake ya bidhaa za chakula baada ya kususa za ulaya? thubutu! sisi wenyewe cha kukila hatuna uwezo nacho, cha kumuuzia mtu utatokea wapi uwezo? Sijasoma biashara lakini nafahamu vitu vitatu muhimu kuwa navyo ili biashara iwe ya mafanikio, products,markets or a buyer and salesman. Vitu hivi vitatu vyote vikiwa katika ubora wake wa quantity na quality kwanini nchi zetu tushindwe kujiendesha? Lakini Sana utakuta wenye uwezo wa kufanya kazi ile kwa ufanisi wapo lakini mtoto wa fulani asiekuwa na uwezo kaekwa pale badala yake.Au ujinga wa wasomi wetu wakeshapata elimu badala ya kuifanyia kazi kwa vitendo anakuwa boss kwa kuwa anaelimu. badala yeye kuwa mfano na watumishi wengine wajifunze kutoka kwake, sasa watumishi wetu wanaelewa maana na faida ya kusoma ni kuja kubweteka kwenye kiti ukiwaachia wengine wakifanya kazi, lazima tubadilike ni maoni tu.