(Picha zote na Benedict Liwenga)
Na. Benedict
Liwenga.
NCHI
wanachama wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameaswa kuenzi lugha ya
Kiswahili na kuifanya kuwa lugha ya kufanyia kazi katika Jumuiya hiyo.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe.
Daniel Kidega alipofanya Mkutano uliowahusishwa Wabunge wa Mabunge ya Afrika
Mashariki (EALA) lengo likiwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya
hiyo.
Mhe.
Kidega ameeleza kuwa, lugha ya Kiswahili ina umuhimu mkubwa kwa Jumuiya hiyo
ambapo ameshauri kuwa kuna haja ya kupitia katika Sheria ya Bunge hilo ili kuhakikisha
kuwa Kiswahili na Kiingereza vinatumika ama kuzungumzwa kila mahali katika
Afrika Mashariki.
‘’Tupate
muda wa kutumia Kiswahili na kuhakikisha kuwa Kiswahili kinazungumzwa katika
nchi zote za Afrika Mashariki kwani ni lugha ya Afrika na sisi ni Waafrika,
hivyo tutafute namna ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kufanya kazi kwa
Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki,’’ alisema Kidega.
Aidha,
Spika Kidega amegusia suala la watu wenye ualibino ambapo ameeleza kuwa, nchi
wanachama hazinabudi kupiga vita masuala ya ukatili kwa watu wenye ualbino
ambapo amezitaka Serikali wanachama wa Jumuiya hiyo kuhakikisha kuwa Albino
wanaheshimika kama binadamu wengine na kuwachukulia hatua kali za kisheria
wahusika wanaojihusisha na ukatili dhidi ya watu hao, kwani kwa kufanya hivyo
kwa pamoja kutapunguza ama kuondosa changamoto zinazowakabili watu wenye
ualbino.
Mhe.
Kidega hakusita kuwapongeza Wabunge wanachama wa EALA waliohudhuria Semina ya
Siku mbili (3 Machi- 4, 2016) iliyolenga kujadili masuala ya changamoto za
uchaguzi kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo waliweza kujadili kwa undani
baadhi ya changamoto za uchaguzi na madhimio mbalimbali yenye kuleta maendeleo
katika Jumuiya hiyo.
Kwa
upande mwingine, Mhe. Kidega amewaasa Wazanzibar ambao hivi karibuni wanaenda
kupiga kura na kuwataka kufanya uchaguzi huo kwa uhuru na haki ikiwemo kudumisha
amani ya Kisiwani humo pamoja na Tanzania kwa ujumla.
‘’Niwaombe
Wazanzibar ambao mda si mrefu mnaenda kurudia uchaguzi wenu, tiini sheria za
nchi, jitokezeni kupiga kura kwa wingi na hakikisheni kuwa mnafanya uchaguzi wenu
kwa uhuru na haki ili kudumisha amani ya Tanzania, alisema Kidega.
Mhe.
Kidega pia amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John
Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ambayo inabadilisha sura ya
Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa kwa kujituma kwao katika kuwatumikia watanzania wote.
No comments:
Post a Comment