ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 15, 2016

UDOM YAJIPANGA KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA TASNIA YA SANAA TANZANIA.

Stara Thomas (Chief Judge akiwa na Josias Charles Katibu Mkuu Serikali wa Wanafunzi ambaye ni muandaaji wa mashindano)
Kwa kipindi kirefu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wengine wa Sanaa wamekua wakilalamikia kutokusonga mbele kwa Tasnia ya sanaa nchini huku lawama kubwa zikiwa juu ya kukosekana kwa Elimu kwa wasanii nchini Tanzania itakayowawezesha wasanii kuendana na ushindani wa soko la sanaa nchini ña hata Duniani kwa Ujumla.
Kwa kutambua mchango wa Sanaa nchini Tanzania katika kupambana na tatizo la Ukosefu wa Ajira vijana kadhaa ambao pia ni wanafunzi Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wameamua kuingia rasmi katika harakati za kuboresha Tasnia ya Sanaa nchini na tayari wameanza kwa Kufanya Shindano kubwa lililofahamika kama UDOM TALENT SEARCH.
Baada ya shindano hilo la aina take vilipatikana vipaji kadhaa katika Sanaa ya Uimbaji,na Uchezaji(dancers) lakini pia katika upande wa uchekeshaji ambapo muamuko ulikua mdogo kwa kujitokeza washiriki wachache mno.
Baada ya Mashindano hayo Vijana Hawa ambao wote ni wasomi wa Chuo kikuu cha Dodoma waliamua kuungana na kuanza kutengeneza Kazi mbalimbali za muziki kwa nia ya kuelimisha jamii na kuburudisha.


Kwa sasa vijana Hawa wanajipanga na Project moja kubwa itakayokwenda kwa Jina la Mama Africa na inaandaliwa Chini ya Kampuni ya C&S Global Promotion ambayo imesajiriwa Mahususi na ndg Josias Charles kama namna ya kurahisisha kuwasaidia vijana hawa wenye vipaji kuhlfikia ndoto zao na kuachana na utegemezi wa Ajira.
Josias Charles C&S Global Promotion CEO
Kampuni ya C&S Global Promotion ipo chini ya Ndg. Josias Charles ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji na Msanii nguli wa Muziki Tanzania Bi. Stara Thomas ambaye ni Mkurugenzi mkuu Msaidizi ambao kwa pamoja wamejipanga kuhakikisha wanajenga historia mpya Tanzania kwa kuhakikisha wanashirikiana na wadau mbalimbali wa sanaa ndani na nje ya Tanzania ili kuwasaidia vijana wenye vipaji kufikia ndoto Zao.
Katika mazungumzo ya Swahili Media Group (SMG) na Mkurugenzi wa kampuni ya C&S Global Promotion ndg. Josias Charles ametanabaisha kuwa maandalizi kwa ajiri ya Project ya "Mama Africa " yanaendelea vizuri na kuwa hadi hivi sasa Tayari "Wimbo maalumu kwa ajiri ya Mama Afrivmca umesharekodiwa na moja wapo ya Studio kubwa mjini Dodoma na mida wowote utaanza kupigwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini.
Mkurugenzi Huyo ametoa wito kwa wadau wote wa Sanaa kokote Duniani kuhakikisha wanajitokeza kuunga mkono harakati hizi za kuwakwamua vijana wa kitanzania na ukosefu wa ajira na umasikini. Na kwa taasisis,Makampuni, ama MTU mmoja mmoja atakayependa kudhamini tukio la Mama Africa anaweza kuwasiliana kwa namba 0766935721 au email josiasycharlesy@gmail.com ili kupata utaratibu mzima wa udhamini na namna mdhamini atakavyonufaika na mradi huu.
Source. Swahili Media.

No comments: