Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini,
Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini na mshereheshaji wa kongamano hilo, Amon Manyama akizungumza katika kongamano la vijana na maendeleo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam limefanya kongamano la vijana na maendeleo kujadili jinsi vijana wanavyoweza kutumika kusaidia kuleta maendeleo nchini na kubadili mfumo wa vijana katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi.
Akizungumzia kongamano hilo limelofanyika siku ambayo UNDP imetiza miaka 50 tangu kuanzishwa, Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini, Amon Manyama alisema kuwa vijana wana nafasi kubwa katika jamii na kama wakitumika vizuri wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo na hivyo kupitia kongamano hilo wanataraji kuwapa mbinu mpya.
Alisema mbali ya kuangala jinsi wanavyoweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo pia wanajadili kwa pamoja ili kuona jinsi gani wanaweza kubadili mfumo wa vijana wa kufanya maamuzi ambao wengi wao wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo baadae yanaonekana kutokuwa sahihi.
“Tunafanya kongamano hili na vijana kutoka vyuo mbalimbali ili kuona mustakabali wa vijana wa Tanzania, kuona jinsi gani wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo Tanzania na hata kubadili mfumo wao wa kufanya maamuzi,” alisema Manyama.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo alisema vijana wana nafasi kubwa kusaidia uapatikanaji wa maendeleo nchini na wao kama UNDP wamekuwa wakisaidia na serikali ili kuwasaidia vijana kwa kuwapa mbinu ambazo wanaweza kutumia ili kufikia malengo waliyonayo.
Alisema licha ya kuwepo changamoto zilizopo katika sera ya vijana lakini pia vijana wamepoteza udhubutu wa kufanya maamuzi na hivyo kongamano hilo wanaweza kukuza uwezo wao wa kujiamini na kufanya maamuzi ambayo yanakuwa ni sahihi.
“Vijana wanatakiwa kuwa na malengo na kukuza uwezo wa kujiamini … vijana wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo Tanzania na wana hamasa ya kusaidia kupatikana maendeleo hivyo wanatakiwa kupewa nafasi katika kufanya maamuzi,” alisema Bi. Dabo.
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini,
Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo,
kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Sehemu ya vijana kutoka vyuo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo wakati akitoa neno la ufunguzi wa kongamano hilo.
Kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Uchumi, Jehovaness Aikaeli alisema vijana wanaweza kutumiwa kama fursa hasa katika kipindi hiki ambacho kunakuwa na vijana wengi ambao wanatoka vijijini na kukimbilia mijini na hivyo kama wakishirikishwa wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo.
Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jehovaness Aikaeli akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano hilo.
Nae mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina alisema mifumo inayotumika sasa nchini inawabana vijana kusaidia kupatikana kwa maendeleo na kama watakuwa wanataka vijana wahusike kikamilifu basi wawatolee vikwazo vinavyowabana kushiriki akitolea mfano katika ajira kwa ajili wengi kutaka wafanyakazi walio na uzoefu mkubwa wa kazi jambo ambalo ni ngumu kupata vijana.
Mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina.
Benedict Kikove kutoka Ubalozi wa Japan nchini akiwaelezea vijana fursa zilizopo kwa vijana na changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kongamano la vijana na maendeleo lililoandaliwa na UNDP.
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akifuatilia kwa makini kongamano la vijana na maendeleo.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) nae alikuwa ni miongoni mwa watoa mada katika kongamano hilo.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (wa kwanza kulia) akifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika kongamano hilo lililoandaliwa na UNDP.
Fatma Mohamed kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV) akizungumzia changamoto wanazokutana nazo vijana katika kutafuta mafanikio.
Mwakilishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kutoka Zanzibar, Saleh Mubarak akielezea washiriki jinsi serikali inavyowasaidia vijana katika kongamano la vijana na maendeleo.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambao ni vijana na wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali nchini lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Afisa wa Utawala Bora kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Godfrey Mulisa akielezea jinsi washirika wa maendeleo wanavyotoa fursa kwa vijana na jinsi fursa hizo zinavyoweza kuwasaidia vijana wa Tanzania.
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Pichani juu na chini ni vijana kutoka vyuo mbalimbali nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye kongamano hilo.
Makamu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Titus Osundina akitoa neno la hitimisho la kongamano la vijana na maendeleo.
No comments:
Post a Comment