ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 11, 2016

Waziri Mahiga na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son waelezea lengo la ziara ya Rais wa Vietnam nchini Tanzania


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitoa taarifa kuhusiana na dhima ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang nchini Tanzania na manufaa yake kwa pande zote mbili, leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son akieleza makubaliano waliyofikia ya ushirikiano baina ya Tanzania na Vietnam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang nchini Tanzania na manufaa yake kwa pande zote mbili, leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Wizara toka pande mbili za Tanzania na Vietnam pamoja na Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) pamoja na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son wakipeana mikono ya shukurani mara baada ya kumaliza kutoa taarifa zao kuhusiana na makubaliano yaloiyofikiwa kati ya Tanzania na Vietnam kuhusiana na ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang nchini Tanzania iliyoanzia tarehe Machi 8 - 11, 2016 Jijini Dar es Salaam.



(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)



No comments: