ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 30, 2016

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAANZA VIKAO VYA MAPITIO YA RASIMU YA BAJETI YA WIZARA HIYO KWA MWAKA 2016/17

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi la Polisi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia meza kuu) katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi la Polisi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Kitwanga, ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia) alipokuwa anamfafanulia jambo katika kikao cha kupitia Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 ya Jeshi lake. Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi la Polisi katika Wizara yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifuatiwa na Naibu IGP, Abdulrahman Kaniki. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi

No comments: