ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 7, 2016

Baada ya kufika Rwanda, Rais Magufuli kapewa hii zawadi na Rais Kagame


Baada ya Rais Magufuli kufanya uzinduzi wa kituo cha pamoja cha maswala ya Uhamiaji kitachokua kina Maafisa wa uhamiaji wa Tanzania na Rwanda kwa pamoja (jengo la pamoja litalofanya kazi za uhamiaji kwa nchi hizi mbili), na kuzindua daraja la kimataifa vyote hivyo vikiwa mpakani mwa Tanzania na Rwanda, alielekea Rwanda kuendelea na ziara yake.


Unaambiwa Rais Kagame alimkaribisha Dr. Magufuli kijijini nyumbani kwake na kumzawadia Ng’ombe watano kwa mujibu wa Mwandishi wa habari Kebendera waRadio na TV ya Taifa Rwanda, ambapo anasema kwa Rwanda ni heshima kubwa sana unapozawadiwa Ngo’mbe.

Rais Magufuli na Rais Kagame nyumbani kijijini kwa Rais Kagame nchini Rwanda, picha imepigwa na ofisi ya Rais Rwanda.

Mwandishi Kabendera anasema ‘Sikumbuki kama kuna Rais aliwahi kuitembelea Rwanda akazawadiwa Ngo’mbe kama Dr. Magufuli, hii imemaanisha ni urafiki tena ule urafiki wa ndani, Rais Kagame ameonyesha undugu na urafiki tofauti na alivyofanya kwa Marais wengine’

Kabendera anasisitiza zawadi ya Ng’ombe ni zawadi yenye thamani sana nchini Rwanda, kugawiana Ng’ombe ni kitu kimekuwepo toka enzi za mababu, mtu anayekuzawadia Ng’ombe ni mtu anaekupenda sana na kukuheshimu, Wanyarwanda wameitafsiri hii kama undugu na urafiki tofauti na anavyofanya Rais Kagame kwa Marais wengine. Credit:Millard:Ayo





No comments: