ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 8, 2016

BOSI WA ZAMANI WA TRA HARRY KITILLYA, SHOSE SINARE NA SIOI SOLOMONI WANYIMWA DHAMANA

Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya, akipunga mkono kwa baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo wamerejeshwa rumande.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Dhamana yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao.
Dk. Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu.

Upande wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa haramu uliosababisha watuhumiwa hao kukosa dhamana. Tibabyekonya ameieleza mahakama kuwa, shitaka la utakatishaji fedha halina dhamana.

Upande wa utetezi ulifanya mapitio ya kesi mbalimbali zinazofanana na kesi hizo ikiwemo kesi namba 314 ya mwaka 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa ya Mwanza iliyokuwa ikimkabili Kigunda Francis aliyeshitakiwa kwa kosa kama hilo lakini alipewa dhamana.

Christopher Msigwa, wakili wa serikali amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa sababu, kosa hilo linaathiri uchumi wa taifa.

Washitakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande hadi tarehe 22 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani, Shose Sinare akisindikizwa na Askari wa Jeshi la Magereza kwenda kwenye gari maalum, tayari kwa safari ya kurudishwa rumande baada ya kesho yao kusogezwa mbele.
Sioi Solomoni akijiangaa kupanga Gari hilo.



8 comments:

Anonymous said...

Siio mask hard duh!

Anonymous said...

Maskini sioi mtoto wa watu .arranged marriage Kati ya mtoto wa waziri na waziri matokeo Yake haya .lowasa kamtumia sioi .

Anonymous said...

Sawa sawa hii ndio Tanzania mpya tunayoitaka. Dhamana ya Nini? Na hao wamejijazia mihela ya wizi kwa kuwaibia Taifa hili. Ni mmja kwa mmja jela

Anonymous said...

Kwenda kule unamoungia nani mkono, jambazi mkubwa weee

Anonymous said...

Is that really a bus to carry people. Seems to be rusting and never washed for ages. Wafungwa nao ni watu jamani. From boss TRA to that, hapo iko kazi Bongoland

Anonymous said...

Acha nao waonjeshwe maisha ya kijehanamu wanayoyaishi wananchi walalahoi wa Bongo!

Anonymous said...

Akanywe wine Za Mchicha huko Keko

Anonymous said...

Sioi ametoka kwenye family nzuri ila mambo ya kuendekeza ushauri wa wazazi.mtoto wa Lowasa mwenyewe ulioa kwa kulazimishwa.Sioi una akili za darasani ebu achana na Hao wakina Lowasa .tukusaidiaje sasa Hapo .lowasa used sioi .sio Mungu akulinde aisee