Hotuba ya kwanza ya Rais Magufuli nje ya nchi, yupo Rwanda. (Dakika 7)
3 comments:
Anonymous
said...
Anachokifanya Magufuli kinavutia sana kwani kuimarisha ujirani mwema na hasa ukichukulia yakuwa Tanzania ni mlango mkuu wa kuingilia kwa nchi kama Rwanda,Uganda,burundi,Malawi,zambia,DRC. Tanzania tumechelewa na tulikuwa tunacheza na maisha kwani kama tungeekeza kwenye bandari zetu kikamilifu na kuzishawishi nchi hizi kutumia bandari zetu katika kupitishia mizigo yao kikamilifu basi hivi sasa tungekuwa mbali sana. Kwanini baadhi ya nchi hizi zinatumia bandari za mbali kama vile Southouth Africa au Mozambique au hata kenya na kuziacha bandari zetu sababu ni kila mtanzania anajua. Vitendo vya wizi katika bandari zetu,ucheleweshaji,utozaji wa ada zisizo na mpango,miundo mbinu mibovu,usalama m'bovu katika njia ambazo zinatumika kusafirishia hizo bidhaa nakadhalika nakadhalika. Mdau hapa kutoka marekani mwanadiaspora sina uhakika kama Magufuli au wapambe wake wanafuatilia vijimambo wakipata wasaa kwani ni moja ya kiota kikubwa cha maoni na mawazo ya wanadiaspora tuliokuwepo huku nje. Maoni ni maoni yanaweza yakawa yakufuraisha na yamaana na vile vile yanaweza yakawa ya kuchukiza na yana maana ndani yake au hata yakawa kuchukiza na ya hovyo kabisa. Lakini hapa mimi ninachotaka kukizungumzia ni maoni ya maana na yakizalendo kwa nchi yetu. Na ujumbe huu ni kwa muheshimiwa Magufuli(An African Super Star President) ingawaje naelewa analifahamu hili ninalotaka kulizungumza zaidi ya mara elfu moja kuliko mimi. Zanzibar ilikuwa maarufu na kuwa kituo kikubwa cha biashara katika miaka ya nyuma kuliko nchi yeyote ya east na kati mwa Africa sababu ya bandari . Tanzania imeshindwa kutumia mazingira mazuri ya nchi yake kuzitumia bandari zake kuwa kituo kikubwa cha biashara katika ukanda wa Africa mashariki na kati. Kwanini wakenya watupite? Nnaimani kabisa kama Tanzania inakuwa makini katika kudumisha huduma bora kabisa za bandari na kufika kuzishawishi nchi jirani kutumia bandari zetu kikamilifu basi tutazungumzia 24/7 day and business katika bandari zetu na ikiwa hivyo hapo tunazungumzia uzalishaji wa ajira kwa watanzania hasa daresalam. Vile vile biashara katika maeneo ambayo malori ya usafirishaji wa mizigo yanapita yaani motels na hotels na restaurants hizo zote ni ajira. Biashara ni ushindani na katika hili suala bandari katika kuhudumia nchi jirani tukubali tumechemsha lakini tujiulize tutakuwa wazee wa kuchemsha sio wa kuivisha mpaka lini? Tunatakiwa kujitahidi kukimaster kisawa sawa japo kitu kimoja ama kilimo au biashara au viwanda au hata uhalifu?ndio hata uhalifu. Wataliana walisifika na kujipatia umaarufu na kuiletea heshima na utajiri nchi yao kwa vitendo vya kihalifu, japo heshima ya kipuuzi lakini heshima ni heshima. Sisi watanzania hakuna tulichokimaster zaidi ya porojo. Mimi naona kwa sasa Bandari ndio mpango wenyewe hata tukimnyanganya mkenya tonge yake ya bandari si tatizo kwani nafasi ya ukaribu wa nchi jirani na Tanzania ambazo zinahitaji huduma za bandari kama zingekuwa karibu na kenya basi bandari zetu hivi sasa tungekuwa tunauzia dagaa. Kwa Tanzania tunatakiwa kuwa very aggressive,very hungry katika kuhakikisha sisi tunaongoza katika kuzihudumia nchi jirani katika huduma za bandari na manufaa yake tutayaona katika kipindi kifupi sana kijacho . Kwani kujenga miundo mbinu ni kuzalisha ajira,sasa tunalia na ajira tuna maeneo mapana kabisa ya kuzalisha ajira zikalipa kwa kipindi kifupi kabisa. Upanuzi wa kazi wa bandari zetu utazalisha ajira za upanuzi wa miundo mingine bara bara nakadhalika,ajira za usafirishaji nakadhalika nakadhalika.
"Tunatakiwa kujitahidi kukimaster kisawa sawa japo kitu kimoja ama kilimo au biashara"
Marahaba Anon#1, Bandari zenye uwezo mmkubwa zitatuwezesha kukimaster kitu kimoja: BIASHARA.
Nchi yenye mfumo wa kujenga biashara imara itaweza kukamilisha malengo yake yote iwe elimu, ajira, afya, mazingara, uchumi, n.k. Ndugu JPJ Magufuli tunahitaji mazingara yanayo unga mkono kwa uthabiti kabisa uimarishwaji wa biashara zilizopo sasa na ujenzi wa biashara zingine mpya kufikia angalau biashara elfu saba (7000) za kiwango cha kuweza kuuza bidhaa na huduma zake ndani ya nchi lakini la muhimu zaidi biashara hizo ziwe na uwezo wa kuuza bidhaa na huduma zake nje ya nchi ili uchumi upanuke zaidi (na hapohapo ajira itaongezeka).

But those cows are given to him as the President, so they belong to the state not to him
Post a Comment