ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 12, 2016

'Sikupendi wala sikuzimii Marekani'- Diamond


Msanii Diamond Platnumz amefunguka kuhusu suala la yeye kutonunua nyumba nchini Marekani kama wasanii wenzake wakubwa wa Afrika wanavyofanya.

Diamonda amefunguka hilo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa haoni umuhimu wa yeye kununua nyumba Marekani, tofauti na alivyonunua Afrika Kusini, kwani kule ilimlazimu.
“Nna nyumba South Africa kwa sababu nina familia South Africa kwa hiyo ni lazima ninunue nyumba south Africa, lakini sina sababu ya kusema ninunue nyumba Marekani, ninunue nyumba Marekani kwa sababu gani, kwanza sipapendi, uongozi unajua kabisa”, alisema Diamond.

Pia Diamond aliweka wazi kuwa kununua nyumba Marekani kwake hakuna faida, ni heri awe na kijiji cha nyumba Tandale au Mwananyamala, lakini si Marekani.

“Nyumba sio hela nyingi dola laki mbili kama milioni mia nne unanunua nyumba, so ni matakwa ya mtu mwenyewe, sasa usitake kununua nyumba Marekani wakati trip zako za kwenda Marekani ni chache, usitake kuonekana tu una mashauzi, mara kumi milioni 500 ukanunua nyumba pale Tandale karibuni 10 ukapost nna kijiji Tandale ukazipangisha ukaingiza hela kuliko Marekani”, alisema Diamond.

9 comments:

Anonymous said...

Point uliongea ya mwisho ina make sense ila kusema nyumba ni laki mboli tu hiyo inaonyesha wazi huna uelewa kuhusu nyumba za Marekani. Watu wengi wana pesa kutoka nchi nyingine lakini kununua nyumba Marekani kama wewe siyo mkazi siyo hatua ndogo.Na nyumba ya laki mbili mara nyingi ni miji midogo au country juu ya yote hiyo nyumba ya laki mbili ni ya sisi walala hoi siyo nyumba wa staa mkubwa. Waulize wenzako kwanza.

Anonymous said...

nimependa kweli usemi wako Diamond na umeongea kitu cha kweli kumbe una akili ya maisha na pia leo na kesho umenunua nyumba marekani umeharibu kidogo ukazuiliwa kuingia lkn kijiji chako tandale wewe unapeta kwenu ni kwenu..BIG UP

Anonymous said...

Hahaha eti ukazuiliwa kuingia lmaoooo

Anonymous said...

Huwezi kununua nyumba yako ukaharibu ukanyimwa kuingia.kwanini uharibu na utaharibuje? Hebu tuelimishe maana tuna nyumba USA miaka mingi sijasikia hii.Pia sio rahisi Diamond kununua nyumba USA hata angetaka kwa vile kigezo sio tu pesa za nyumba.

Anonymous said...

Hahahahaha... Zizitaki mbichi hizo. We kaa kwenye kijiji cha tandalae. it make sense to know your limitation.. Unyamwezini utaazirika tu mjomba. Dola laki mbili ni townhouse tena in a acountry side, if you do that ustaa wako unoimarishwa na watu wa bod boda will never be replicated in the US. Hata mimi natamani nipate nyumba US lakini I can't afford kwa hiyo nitajibanza na wewe hapa hapa Tandale -what you are saying is like me saying I am not going to attend Messis's pool party even if he invites me -the point is I am not invited period.. Stay real and for that I salute you.

Anonymous said...

Wote mlio mpongeza Diamond hamnazo. Hivi wewe kwa mawazo yako unadhani Diamond anapeza zakununua nyumba Marekani au ni kujishaua tu. Akija kiingilio tu ni $10-20 watanzania wenyewe hawafiki hata 200 kwenye Hall. Mziki anaongea kimakonde. Acha kuwadanganya watoto wa kibongo waende shule. Asingekuwa anaipenda Marekani hasingekuja mara kwa mara kama mzee wa bagamoyo.Yes anaweza kuwa na nyumba Marekani kama atakuwa na credit nzuri au CASH...na si maneno maneno au vijisenti laki mbili kama alivyo zungumza. Labda kama anazungumzia maeneo yanayofanana na Tandale hapo sawa. Na hata hivyo hawezi kutoa cash $200,000. Wewe umempata huyo msous/mganda tulia hacho urongorongo.

Anonymous said...

Diamond nyumba ya dola laki mbili ni unanunua townhouse or condo tena ni miji midogo. Kama unataka ku-level as super star uliza nyumba kwenye miji mikubwa kama New York, Washington, California etc. Naomba investment advisor wako akupe shule ya Real Estate Investment. Real Estate Market ya Tanzania huwezi kulinganisha na nchi kama US for sure. Ku-nunua hizo big mansion za ma-superstar you need some steady income to run through expenses. Hiyo laki mbili inawezekana na expenses za mwezi kwenye nyumba.

Anonymous said...

Diamond wewe ni star unakaaje nyumba ya laki 2 marekani? Sisi ndio tuna kaa hizo na tupo nje ya mji, laki 2 hujanunua nyumba ya mjini, lkn waweza nunua ya tandale ya marekani. Kama unampango wa kukaa tandale ya marekani means getto, then nunua nyumba ya laki 2

Anonymous said...

Diamond, usijali wasemavyo walimwengu. Kuna wanao kupenda na kuna wanao kuchukia. UMETOKA mfano umekuwa mbaya, na huna pesa. Wenye kukudharau, acha wakudharau, ila watakuja kuona umuhimu wako uko wapi hapo baadae. Pia napenda nikushukuru kwa kuinua vijana wenzio kwa kuwa support. Mwenyezi Mungu akuzidishie, na azidi kukupa moyo huo huo wa kuwasaidia wengine. Inshaallah!