Advertisements

Thursday, April 28, 2016

SUKARI: MTIHANI WA KWANZA SERIKALI YA MAGUFULI KUFELI

By Malisa GJ,
Takribali Miezi miwili iliyopita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli alipiga marufuku uingizwaji wa sukari nchini kwa madai ya kusaidia kulinda viwanda vya ndani vinavyozalisha biidhaa hiyo nchini. Rais Magufuli alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wafanyabiashara ambapo alitaka agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja.

Baada ya utekelezaji wa agizo hilo kuanza kumejitokeza mfumuko mkubwa wa bei katika bidhaa ya sukari ambayo imepanda kutoka Shilingi 1,800/= kwa kilo moja hadi shilingi 2500/- huku baadhi ya maeneo ikifika shilingi 2800/-. Ongezeko hili ni wastani wa asilimia 39% hadi 55% kwa kilo moja ya sukari. Yani mfumuko wa bei ya sukari umefikia asilimia 55% ndani ya kipindi kisichiozidi miezi miwili. Hii ni ishara mbaya sana kiuchumui (Indicator for galloping inflation).

Kwanini Rais alizuia sukari kutoka nje?
Rais Magufuli alipiga marufuku uingizwaji wa sukari ya nje ili kuilinda viwanda vya ndani. Kiuchumi bidhaa kutoka nje inaweza kuathiri viwanda vya ndani (infant industries) vinavyozalisha bidhaa kama hiyo, hasa ikiwa bidhaa hizo za nje zitauzwa kwa bei ndogo kuliko zinazozalishwa nchini. Hii inaitwa Protectionism theory.!

Kwa hiyo lengo la Rais Magufuli bila shaka lilikuwa jema lakini alishauriwa vibaya. Katika soko la uchumi huria bei ya bidhaa haipangwi na Rais bali nguvu ya soko (market forces). Nguvu ya soko ndiyo inayoamua leo bidhaa iuzwe bei gani. Kuna viashiria vingi (determinants) vya nguvu za soko ambavyo hutumika kupanga bei ya bidhaa. 

Vishiria viwili vikubwa ni uzalishaji na usambazaji wa bidhaa (production &supply) na cha pili ni mahitaji ya bidhaa husika (demand). Vigezo hivi ndivyo huamua bei ya bidhaa. Maana yake ni kwamba ?market forces? zina nguvu kuliko Rais au Waziri Mkuu. Hakuna mtu aliyewahi kushindana na ?market forces? akashinda, hata kama akiwa adikteta. Muulize Mugabe analifahamu hili vizuri.

Namna Kanuni hizi zinavyofanya kazi.
Kwa kawaida bidhaa ikiwa nyingi sokoni (higher supply), mahitaji (demand) hupungua na bei (price) pia hupungua.  Kwa mfano msimu wa machungwa, mahitaji ya machungwa hayawi juu kwa sababu watu wana uhakika wa kuyapata muda wowote wakitaka. 

Hivyo basi bei ya machungwa itashuka sana kwa kuwa machungwa ni mengi kuliko mahitajhi ya walaji. Na ikitiokea bidhaa imepungua sokoni kuliko mahitaji ya walaji, hufanya mahitaji ya bidhaa hiyo kuongezeka na kusababisha pia bei kupaa. Hizi ni miongoni mwa kanuni rahisi sana za uchumi ambao viongiozi wetu wanapaswa kuzijua (Basic Micro Economics insights).

Nini kilitokea?
Bahati mbaya Rais alipopiga marufuku uingizwaji wa sukari nchini hakuzingatia kanuni hizi, na washauri wake hawakumshauri juu ya hili. Kwa takwimu za wizara ya viwanda na biashara, matumizi ya sukari nchini ni wastani wa tani 420,000 kwa mwaka. Lakini wakati Rais anapiga marufuiku uingizwaji wa sukari, kiwango kilichokuwa kinazalishwa na viwanda vyote vya ndani ni tani 300,000 tu. 

Maana yake ni kwamba tulikuwa na upungufu (deficit) wa zaidi ya tani 100,000 ambazo tungeweza kuagiza kutoka nje ya nchi ili kuziba hilo pengo. Lakini bahati mbaya washauri wa Rais wakamuaminisha kwamba viwanda vya ndani vinaweza kuzalisha tani zote 420,000 na kuondoa mahitaji ya kuagiza sukari kutoka nje.

Kwa hiyo Rais akaagiza sukari yote izalishwe kwenye viwanda vya ndani. Yani viwanda vyetu vianze kuzalisha tani 420,000 sawa na mahitaji ya walaji. Bahati mbaya Rais hakutaka kujua kwanini viwanda vyetu vilikuwa havizalishi kwa kiwango hicho. Kuna mambo mengi yanayofanya viwanda vya ndani kuzalisha tani 300,0000 kwa mwezi. Kwa hiyo ni vema Rais angesikiliza sababu hizo kwanza, kabla ya kukimbilia kuagiza vizalishe kwa kiwango hicho.

Rais Magufuli angeuliza kwanza kwanini viwanda vya ndani vimeshindwa kuzalisha sukari inayokidhi mahitaji ya soko la ndani. Baada ya kusikiliza sababu hizo achukue hatua ya kuzifanyia kazi kabla ya kuagiza wazalishe kwa kiwango anachotaka.

Baaadhi ya sababu zilizofanya viwanda vya ndani kushindwa kuzalisha na kukidhi soko la ndani ni pamoja na upungufu wa mashine za kisasa katika viwanda vya uzalishaji, teknolojia duni, ufinyu wa bajeti, upungufu, upungufu wa mali ghafi na upungufu wa rasilimali watu.

Viwanda ambavyo vinatumia mashine za kale, taknolojia duni, na watumishi walewale haviwezi kuzalisha tani 420,000 kwa sababu tu Rais ametoa agizo. Bahati mbaya agizo la Rais haliwezi kuzidi nguvu ?marketing forces?. Agizo la Rais halina nguvu kushinda "Demand &Supply Theory"

Athari za Agizo la Rais.
Kutokana na sababu hizo hapo juu, viwanda vimeshindwa kuzalisha kufikia kiwango cha tani 420,000 kama Rais alivyoagiza. Wakazalisha wastani wa tani 300,000 lakini mahitaji halisi yakiwa tani 420,000. Maana yake ni kwamba mahitaji ya sukari ni makubwa kuliko kiasi kinachozalishwa. 

Kwa kuwa kiasi kinachozalishwa (supply) ni kidogo kuliko mahitaji (demand) ya walaji, ni lazima bei ipande maradufu. Kanuni za uchumi zinasema ?The Low the supply, the higher the quantity demanded and the higher the price? yani ikiwa bidhaa itazalishwa kwa kiasi kidogo na mahitaji yakawa makubwa ni lazima bei itapanda maradufu. Na hivi ndivyo ilivyotiokea kwenye suala la sukari nchini. Uzalishaji ni mdogo ( tani 300,000) lakini mahitaji ni makubwa (tani 420,000).

Lakini bahati mbaya washauri wa Rais wakaendelea kumpotosha kwamba kuna watu wameficha sukari na hivyo kusababisha iuzwe bei kubwa. Ukweli ni kuwa sukari inawezekana ilifichwa kutokana na upungufu uliojitokeza na hivyo kuibua suala la "black market" ambayo ni vigumu sana kuigundua. Maana yake ni kwamba kuna wafanyabishara walificha sukari ili ikizidi kupanda bei ndipo wauze bei kubwa zaidi (maximization of ptofit), na wananchi wachache wakaficha sukari yao ya akiba ili ikipanda bei wasiathirike (hawa ni wale wa matumizi ya nyumbani).

Maana yake ni kwamba hoja ya kwamba kuna watu wameficah sukari sio kiini cha tatizo. Ni matokeo tu. Kiini cha tatizo ni uzalishaji mdogo kulinganisha na mahitaji. Lakini hoja hii Rais alipelekewa na wasaidizi wake ili wajiondoe kwenye lawama za kumshauri vibaya mwanzoni. Washauri wake hawakutaka kuwa wakweli kwamba wao ndio kiini cha tatizo kwa sababu walimshauri Rais kuzuia sukari ya nje wakati viwanda vyetu havijajipanga kukidhi mahitaji ya soko.

Nini kifanyike?
Jambo la kwanza na la msingi ni kuruhusu uingizaji wa sukari kutoka nje ili kuziba pengo la wastani wa tani 100,000 ambalo limejitokeza tangu serikali ipige marufuku sukari kutoka nje. Sukari ikiingizwa itaziba ombwe la upungufu na hivyo kuondoa ile ?marketing competition? ya watu wengi kupigania bidhaa kwa sababu zipo chache. 

Maana yake ni kuwa kiasi cha sukari kitakachokuwa nchini kitakuwa sawa na mahitaji ya walaji kwa hiyo hakutakuwa na ushindani mkubwa wa bei. (The higher the supply, the low the quantity demanded hence the low the price). 

Katika hili nimpongeze Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ameliona hilo na ameweza kuchukua hatua kwa kuruhusu sukari kuagizwa kutoka nje. Hii inaweza kutumiwa kama mbinu ya muda mfupi wakati tuikijipanga kama taifa kutafuta mbuinu za muda mrefu.

Mbinu ya muda mrefu ni kujenga viwanda vingine vya sukari ili visaidiane na vilivyopo katika kufanya uzalishaji wa sukari ya kutosha. Viwanda vilivyopo kwa sasa vimezidiwa. Mahitaji ni makubwa kuliko kiasi kinachozalishwa. Kwa hiyo serikali ikijenga viwanda vingine hata viwili vitasaidia kupunguiza ombwe la upungufu wa sukari nchini.

Mbinu nyingine ya muda mrefu ambayo inaweza kutumika ni kuvisaidia viwanda vya sukari vilivyopo kwa kuviongezea nyenzo, kukuza teknolojia yao, kuwaongezea rasilimali watu na kuvipa ruzuku ili viweze kuzalisha kwa wingi na kwa gharama nafuu. 

Serikali ikikubali kuchangia gharama za uzalishaji kwa viwanda vinavyozalisha sukari kwa kuvipa ruzuuku, ni dhahiri itafanya sukari kuuzwa bei nafuu. Lakini pia serikali kusaidia nyenzo, teknolojia na rasilimali watu itasaidia kuongeza kiwango cha uzalishaji (quantity). Kwa hiyo tutazalisha sukari nyingi ya kutosha kwa mahitaji yetu, tutauza kwa bei nafuu na tutapata "surplus" ya kuuza nje ya nchi.

1 comment:

Anonymous said...

Naona umejitahiti ku quote kila principles za economics,lakini kitu kimoja umeshindwa kutambua ni kuwa biashara hii ya sukari ilikuwa imevamiwa na wahujumu uchumi ambao sio tu walikuwa wana benefit kutokana na faida kubwa ya sukari waliyokuwa wakiagiza,vilex2 walikuwa wana sabotage local industries.
at the end of the day tunge end up kuwa na another ATC, TAZARA, TTCL,UDA in the sugar industry. Worse enough walikuwa hata kodi hawalipi.
Bravo Magufuli, with time tutafika..