
Ndugu Wanaudasa,
Ninasikitika kuwataarifu habari za msiba wa Dk. Richard
Mgaya wa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta kilichotokea usiku wa
kuamkia jana. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara (Dk. Honest Kimaro) kifo cha
Dk. Mgaya kimesababishwa na ajali ya gari.
Siku ya jana kulisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii za
gari lilipopata ajali eneo la Mbezi Afrikana baada ya kugongana na lori
na kuwaka moto.
Mashuhuda walishuhudia gari likiwaka moto na hivyo
dereva aliungua moto na kuteketea na hakuweza kutambulika. Hivyo watu
wakasambaza ujumbe kwa kutaja plate number za gari lililoungua ili
kutafuta utambulisho wa dereva.
Kwa masikitiko makubwa, imejulikana kwamba dereva wa gari
hilo alikua ni Dr. Richard Mgaya. Idara ya Sayansi na Uhandisi wa
Kompyuta na jamii ya CoICT kwa ujumla imeshtushwa sana na msiba huu.
Dk. Mgaya alijiunga na idara yetu miaka kama minne hivi
iliyopita akitokoea masomoni Marekani na alikua ni mtaalamu kijana wa
Artificial Intelligence ambayo ni moja ya specialities za computer
science zenye wataalamu wachache sana wa kiwango cha PhD hapa nchini
mwetu (kama wapo zaidi ya yeye).
Taarifa za kwamba aliyeungua kwenye
gari hili alikua ni Dr. Mgaya zimeifikia familia yake leo mchana.
Pamoja na ujumbe huu, nimeambatanisha baadhi ya picha zilizopigwa eneo la tukio. Ni msiba mgunu sana kuuelezea na kuukubali.
Mungu mwenyewe awe faraja kwa ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake na familia nzima ya UDSM.
1 comment:
Ametangulia mbele ya haki na sisi pia muda wetu ukifika utakwenda !pole ni sana wote tulioguswa na msiba huu ! Mungu awape subira , imani na uvumilivu poleni nyote !
tatizo laajali kwa Tanzania nikubwasana kinyume na tunavyo lishughulikia ! ifike wakati sasa zitungwe sheria zitakazo saidia kupunguza hizi ajali ! mfano basi lina pata ajali watu wana poteza maisha na wengine wanapata vilema ! iwekwe sheria kila gari liwe na bima ambayo ukisabisha ajari kama umepoteza maisha ya mtu au umemsababishia kilema ! yule ulie mgonga anatakiwa amlipe muathilika wa hiyo ajali pesa nyingikuli ngana na kilema alicho msababishia ! kama hilo gari lako halikua na hiyo bima inabidi mali zako ziuzwe ili ulio wagonga walipwe kama hauna kitu unakwenda jela ! ughaibuni dereva ana mkwepa mtu ili asimgonge , lakini bongo mtu analikwepa gari ili lisimgonge ! ifikie wakati gonga lipa pesa kulingana na umemsababishia mtu kilema kiasi gani kama hata fanya kazi maisha hiyo bima ita mlea kama hukua na hiyo bima unafilisiwa mali zako na jela juu !
Post a Comment