ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 28, 2016

WAGENI WAANZA KUWASILI KONGAMANO LA DICOTA 2016 DALLAS, TEXAS NCHINI MAREKANI

Kulia ni Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na mkewe Marystela Masilingi (Wanne toka kushoto) wakimkaribisha Balozi Anisa Mbega  (wapili toka kushoto) anayeshughulikia maswala ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa siku ya Alhamisi April 28, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency ambako ndiko litakapofanyika Kongamano la DICOTA 2016 kuanzia siku ya Ijumaa April 29, 2016.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani akisalimiana na ujumbe ulioongozana na Balozi Anisa Mbega (hayupo pichani) anayeshughulikia maswala ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa siku ya Alhamisi April 28, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency ambako ndiko litakapofanyika Kongamano la DICOTA 2016 kuanzia siku ya Ijumaa April 29, 2016.
Kutoka kushoto ni Nasibu Sareva, Fredrick Mjema, Asha Nyang'anyi, Balozi Anisa Mbega, Mohamed Nuh mwakilishi wa People's Bank of Zanzibar, Emmanuel Kimaryo mwakilishi kutoka CRDB na Lunda Asumani wakiwasili katika hotel ya Hyatt Regency siku ya Alhamisi April 28, 2016.
Uhakiki wa majina ukiendelea.
 Dkt. Allen Rwabutaza kutoka Columbus, Ohio akiwa nje ya hotel ya Hyatt Regency mara tu baada ya kuwasili kwa ajili ya kongamano la DICOTA.
Jackson Munuo kutoka Massachusetts akiwa tayari kwa kongamano la DICOTA 2016.

No comments: