Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na ujumbe kutoka Mtandao Kijinsia Tanzania (TGNP) walipofika ofsini hapo kwa ajili ya kutoa shukrani zao.
Mwanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP),
Bi Gema Akilimali akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani
fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada zilizofanyika katika kuboresha
huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi
wenye kipato cha chini. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco
Mhandisi Cyprian Luhemeja.
WANAHARAKATI WA Mtandao wa kijinsia “TGNP” wamepongeza juhudi
zinazofanywa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco),
kutokana na Mabadiliko na jitihada zinazofanywa na Dawasco za kuboresha huduma
ya Maji pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii inayoizunguka.
Akizungumza katika kikao cha pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni
ya Maji ya “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha
Samwel.
Ameitaka Dawasco kuhakikisha inapeleka huduma ya Majisafi na
salama katika sehemu zote muhimu ikiwamo mashuleni na hospitalini ili
kumpunguzia mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu pamoja na kumuondolea
mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa kutokana na kuhangaika kutafuta Maji.
“Tunataka kutoa salamu za pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko
na jitihada
tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya kusaidia jamii,
tumefurahishwa na jitihada zenu, tutafanya
kazi pamoja ili kuhakikisha tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda
mwingi kuhangaika kutafuta Maji kwani
kampeni yenu ya “MAMA TUA NDOO YA MAJI KICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi.
Martha.
Aidha, Mwanaharakati wa mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali,
amefurahishwa ya kampeni ya Mama tua ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke
kwa kiasi kikubwa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo
ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta
maji, pia anaamini utaongeza ufaulu mashuleni kwani badala ya watoto wa kike
kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa wataweza kuokoa muda na kuwa kushiriki
masomo ipasavyo.
“Wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta Maji, hivi ni saa
ngapi ataleta maendeleo ya nchi? Lazima tumkwamue mama katika janga hili ili na
yeye aweze kujenga nchi yake” alisema Bi. Akilimali.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian
Luhemeja, amehaidi hadi kufikia Disemba 31 watahakikisha kampeni ya mama tua
ndoo ya Maji kichwani itawafikia wakazi wengi wa Dar hususani wale walio katika
tabaka la chini.
Aidha amehaidi kutoa huduma ya Majisafi na salama bure kwa wazee,
walemavu na yatima wote ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kuunganisha
huduma ya Maji, pamoja na kujenga pointi za ya kunywea Maji katika sehemu
mbalimbali za Jiji ikiwa ni pamoja na maeneo ya stendi ya Mabasi ya Ubungo, Buguruni
chama, Magomeni Mapipa na Kisutu stendi ya zamani.
“Mimi pamoja na menejimenti yangu tunaenda kumtua mama ndoo ya
Maji kichwani mpaka kufikia mwishoni wa mwaka huu, kwani Maji yatakuwa mengi
katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam pamoja na Pwani” alimalizia
Mhandisi Luhemeja
No comments:
Post a Comment