ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 27, 2016

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi afungua Mafunzo IRINGA

Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr Ndalichako alifungua mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyo fanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. waliojumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya. 

Mafunzo hayo yana husu uhakiki wa ubora wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu). 
Akifungua mafunzo hayo Dr Ndalichako alisema serikali imepnia kukuza ubora wa elimu inayo tolewa hivyo basi lazima itaboresha kitengo cha uhakiki ubora wa elimu Tanzania. Mkuu wa mkoa akimkaribisha Dr NDalichako alimuomba waziri kuhakiksha Wahakiki ubora wanapewa kipaumbele katika kukuza elimu Tanzania. 
Naye Mkuu wa wilaya bwana Richard Kasesela akitoa salamu alisema " ni wakati muafaka kubadili KKK iliyopo iliyo zoeleka sasa yaani KULA, KULALA na KUCHEZA kuiirejesha kwenye maana halisi ya KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU

No comments: