Basi la Leo Luxury Coach limepata ajali ya kugongana na fuso hapa Manyoni, dereva wa fuso amefariki.
Abiria wa basi wote wazima, inasemekana fuso lilikosa breki wakati likishuka mlima.
Sehemu hii ilipotokea ajali hii inatwa Mbwasa chini ya mlima Sukamahela kuna mteremko mkali na kona kali kama inavyoonekana na mara nyingi madereva wakishamaliza mlima wakiwa wanateremka hua wanaachia breki bila kujali kona ya hapo.
Baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi ilo wakiwasiliana na ndugu na jamaa yao
Fuso likiwa limetumbukia bondeni
No comments:
Post a Comment