Sunday, May 22, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA KILIMO SONGWE, ALITAKA JESHI LA MAGEREZA KUONGEZA UZALISHAJI WA CHAKULA CHA WAFUNGWA ILI KUIPUNGUZIA SERIKALI MZIGO WA KUWAHUDUMIA WAFUNGWA MAGEREZANI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kulia) akioneshwa maeneo mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe, Mkoani Mbeya alipofanya ziara ya kikazi leo Mei 21, 2016 Gerezani hapo(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Songwe, ACP. Laizack Mwaseba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia moja ya shamba la alizeti katika Gereza la Kilimo Songwe.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira(kushoto) akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja kwa pamoja wakiangalia mazao ya mahindi katika Mashamba mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe walipotembelea Gereza hilo leo Mei 21, 2016.
Mahindi yakiwa tayari yamepukuchuliwa na mashine maalum katika Gereza la Kilimo Songwe kama yanavyoonekana katika picha. Gereza hilo hivi sasa linauwezo wa kuzalisha chakula cha kulisha Wafungwa wote waliopo katika Magereza yote ya Magereza Mkoa wa Mbeya.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiangalia mashine ya kupukuchulia mahindi katika Gereza la Kilimo Songwe lililopo Mkoani Mbeya.
Mazao ya Mahindi yakiwa tayari yamevunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe lililopo Mkoani Mbeya kabla ya kupukuchuliwa kwenye mashine maalum.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumusio Achacha akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira alipotembelea Ofisi za Idara hiyo kabla ya kuelekea Gereza la Kilimo Songwe lililopo Mkoani Mbeya(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake