aibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema
Serikali iko katika mchakato wa kuangalia uwezekano wa kubadili matumizi
magari ya polisi ya kuzuia ghasia kwa kurusha maji ya kuwasha maarufu
washawasha yaweze kutumika kuzima moto.
Kauli hiyo ilitokana na
swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliyeuliza
ni kwanini Serikali inanunua magari ya washawasha yasiyo na tija ambayo
hutumika nyakati za uchaguzi tu badala ya kununua magari ya zimamoto.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri Masauni alisema magari ya washawasha bado yana
tija kwani Serikali inafanya taratibu ili magari hayo yatumike kuzima
moto kwenye majanga na isiwe kwa washawasha pekee na kuwataka wabunge
hasa wa upinzani kuondoa fikra za kuyapinga magari ya washawasha kwani
sasa itakuwa ni neema kwao badala ya kutumika kwa kudhibiti vurugu
pekee.
Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana Serikali ilinunua magari ya
washawasha 777 kwa bei ya kati ya Sh150 milioni na Sh400 milioni, hata
hivyo taarifa zingine zilisema magari yaliyotumika wakati wa uchaguzi ni
50.
Awali Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema),
aliuliza swali la msingi kwamba ni lini Serikali itapeleka huduma ya
zimamoto katika mpaka wa Tunduma ili kuokoa mali za wafanyabiashara
wanaosubiri kuvuka pindi ajali ya moto inapotokea.
Naibu Waziri
Masauni alisema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika halmashauri ya Mji
wa Tunduma lina kituo katika eneo la mtaa wa Kilimanjaro, Wilaya ya
Momba katika Mkoa wa Songwe, kinachohudumia wilaya yote ukiwamo mpaka
huo.
Alisema kwa sasa kituo hicho kina gari moja ambalo nalo
liko kwenye matengenezo mjini Mbeya likiendelea kufanya matengenezo huku
askari wakiendelea kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na majanga ya
moto.
Masauni alisema ni azma ya Serikali kupeleka huduma ya
zimamoto katika maeneo ya nchi ikiwamo Tunduma, mpango huo unategemea
upatikanaji wa fedha kwa Serikali.
Kuhusu ujenzi wa kituo cha
Polisi cha Mbozi, alimuomba mbunge wa eneo husika avute subira ili
waweze kuona namna bora ya kufanya kwani bajeti ya Serikali ni ndogo na
vituo vinavyotakiwa kujengwa ni vingi.
1 comment:
Where in the world mmeshaona hilo likifanyika? Acheni magari yatumike kwa malengo yaliyokusudiwa.mkishafanya hiyo convertion then kukaibuka vurugu je,mtatumia magari ya fire kama washax2? Kumbukeni 2020 sio mbali. .
Post a Comment