ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 17, 2016

MAKONDA ASHITUKIA MCHEZO MCHAFU WA KUFANYA GARI ZA SERIKALI KUUZWA.


Na Chalila Kibuda
BAADHI ya watumishi Serikali wamekuwa wakifanya ujanja ujanja wa kuharibu magari ya Serikali ili waweze kutengeneza mazingira ya kuyauza kwa watumishi   hao wa ndani ofisi hiyo  hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitoa magari nane yaliyoenda kutengenezwa na Umoja wa Mafundi Gereji wa Wilaya Kinondoni ikiwa ni kujitolea ili watumishi waweze kutekeleza majukumu yao bila kuleta vizingizio vya kukosa usafiri.

Makonda amesema kuwa gari zinaharibika kitu kidogo lakini hayatengenezwi kwa muda muafaka na kufanya gari hizo kuharibika wakati zikiwa zimegeshwa na baadae kufanya mnada na wanunuzi wa gari hizo ni watumishi.
Amesema kuwa gari hizo zikitengenezwa, na madarevawakiziharibu kwa makusudi basi mshahara wake utakatwa kwa ajili ya kutengeneza gari ambalo limeharibiwa naye.
Aidha amesema kuwa watumishi wanashindwa kuwatembelea wananchi kutokana na kukosa usafiri wakati magari yamekaa kwa muda mrefu na kuendelea kaharibika.
Nae Katibu wa Mfundi Gereji Wilaya ya Kinondoni, Abdallah Rashid amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano na mkuu wa mkoa katika kuhakikisha magari yanakuwepo na watumishi waweze kuwatembelea wananchi kujua matatizo  yao.

No comments: