ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 26, 2016

MPANGO MPYA WA UGAWAJI VYANDARUA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO WAZINDULIWA MKOANI MTWARA

Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara Dr Wedson Sichalwe akionesha moja ya vyandarau vitakavyokuwa vikigawiwa katika vituo vya afya kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wachandarua kliniki, mpango unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi hii na mkuu wa mkoa huo bi halima dendegu. wanao shuhudia kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
mganga mkuu wa mkoa wa mtwara dr wedson sichalwe akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wa chandarua kliniki.pamoja nae walioketi kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
Mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani kuhusiana na zinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima dendego.
Meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi Theresia Shirima, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima dendego.

JITIHADA za kutokomeza malaria nchi zimeanza kuonyesha matunda baada ya takwimu za ugonjwa huo mkoani Mtwara kuonyesha zimeshuka kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012 kitaifa zikifikia asilimia 9 toka asilimia 33.

Takwimu hizo zimeshuka ikiwa ni jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na USAID pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii zinatumia vyandarua vyenye kinga kujikinga na ugonjwa huo ili kuupunguza au kutokomezwa kabisa.

Takwimu hizo zimetolewa na Mganga mkuu wa mkoa, Dk Wedson Sichalwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa chandarua Kliniki utakaozinduliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na mkuu wa mkoa Halima Dendego kwa lengo la kufikisha vyandarua kwa jamii ambao utahusisha wajawazito na watoto wa miezi tisa watakaohudhuria vituo vya afya.

“Tunataraji kuzindua mpango wa usambazaji wa vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kupitia kliniki a wajawazito na watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni mojawapo ya juhudi zinazofanywa na serikali kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha malaria inapungua na madhara yake kwa wananchi,”alisema Sichalwe

Aidha Dk Sichwale alisema katika mwaka 2015 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa yaliyotokana na malaria kwa mkoa huo ni 208,473 ikiwa ni wagonjwa wa nje yani OPD sawa na asilimia 17.5.

Naye Afisa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto, Theresia Shirima alisema ipo mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vyandarua vinafikishwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kupitia shuleni kila mwaka na kwa kaya kila baada ya miaka kadhaa ambayo iliwezesha kufikia jamii kwa asilimia 85 ambayo wanaiendeleza ili kufikia asilimia 100.

“Hatutumia wajawazito na watoto pekee,zipo njia mbalimbali za kufikisha vyandarua kwa jamii, na kwa mkoa wa Mtwara lipo zoezi linaloendelea la kugawa vyandarua shuleni ikiwa ni njia ya kufikia ambayo ni awamu ya nne kwa mwaka wa nne na kwenye kaya tunatoa mara moja baada ya miaka kadhaa ambayo iituwezesha kufikia asilimia 85,”alisema Shirima

Akizungumza mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Albertina Mlolowa aliwataka wanajawazito kuhudhuria kliniki na kupatiwa huduma pasipo kubaguliwa na kusema hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki wakihofia kuulizwa weza wao na kusema suala la afya ya uzazi ni kwa manufaa ya baba na mama.

“Nawaomba kina mama wajawazito wasiogope kuhudhuria kliniki na weza wao kwa faida yao,hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki wakihofia kuulizwa weza wao.lakini watambue suala la afya ya uzazi ni la mama na baba hivyo wanapohudhuria wote kunasaidia kuondoa hatari amabyo inaweza kujitokeza hapo baadae kama maambukizi mapya na wakati mwingine kumsababishia mama kukosa huduma kwa wakati,”alisema Mlolowa

Mpango wa chandarua kliniki unatekelezwa na mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu

No comments: