ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 18, 2016

MSHINDI WA PIKIPIKI DROO NDOGO YA MWISHO SHINDA NYUMBA APATIKANA

Msomaji wa magazeti ya Global akichanganya kuponi kumtafuta mmoja wa washindi.
Msomaji akizidi kuchanganya kuponi hizo.
Msomaji huyo akitaja jina la mmoja wa washindi wa droo ndogo ya mwisho ya Shinda Nyumba.
Kutoka kushoto ni Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda akiwa na Msimamizi Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Chiku Saleh (katikati) na Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli aliyekuwa akiandika majina ya washindi.
Msomaji mwingine wa magazeti ya Global akichanganya kuponi ili kumpata mmoja wa washindi.
Msomaji huyo akimkabidhi MC Chaku kuponi ili ataje mshindi.
Msimamizi Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Chiku Saleh 
(wa kwanza kushoto) akishuhudia jina la mmoja wa washindi waliopatikana baada ya droo ya leo.


Orodha ya majina ya washindi wa droo ndogo ya mwisho ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyochezeshwa leo jioni katika Viwanja vya Bakhresa- Manzese jijini Dar es Salaam.

EVANCE William, mkazi wa Mburahati jijini Dar ameibuka kidedea kwa kushinda pikipiki aina ya Sky Mark kupitia droo ndogo ya mwisho ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyochezeshwa leo jioni katika Viwanja vya Bakhresa- Manzese jijini Dar es Salaam. Washindi wengine ambao walijishindia zawadi katika bahati nasibu hiyo inayoendeshwa kupitia magazeti ya Global Publishers ni Richard Mauga kutoka Kinondoni aliyeshinda Simu ya Kisasa (Smart Phone) huku Hamisi Mwaikambo kutoka Mbeya, Kigodi Rajabu kutoka Dar, Daniel Mligo kutoka Mafinga, Teddy Kasenene wa Dar, Esther Meshack wa Dar wakijishindia Ving'amuzi vya TING. Aidha, Akani Nsemwa kutoka Mbalizi Mbeya alijishindia Dinner Set na Maria N. Mwakale alijishindia Bed Sheet. Baada ya kumalizika droo hiyo ndogo ambayo ni ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba na washindi hao kupatikana, Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda alisema washindi hao watatakiwa kufika katika Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge Jumatano ijayo kwa ajili ya kukabidhiwa zawadi zao. “Waje tu na vitambulisho vyao. Tutawakabidhi zawadi zao. Niwasihi watu waendelee kushiriki bahati nasibu hii kwa kujaza kuponi katika magazeti yetu na kutuma ofisini kwetu kwani droo kubwa ya mwisho itachezeshwa mwezi ujao na mshindi wa nyumba ya kisasa atapatikana,” alisema Mkanda. Droo hiyo inaendeshwa kupitia magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi ya Global Publishers na kudhaminiwa na Kampuni ya Shinyanga Emporium na King’amuzi cha TING. (Picha na Habari: Denis Mtima / GPL)

No comments: