Sunday, May 8, 2016

MWALIMU ADAIWA KUMJAZA MIMBA MWANAFUNZI WAKE WA DARASA LA TANO

Mwalimu wa Shule ya Msingi Tambaruka Kata ya Mkwamba wilayani Nkasi mkoani Rukwa, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumsababishia ujauzito mwanafunzi wake anayesoma darasa la tano katika shule hiyo.

Ofisa wa Elimu ya Msingi Wilaya Nkasi, Missana Kwangulla alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa amekabidhiwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Kwangulla alisema anaandaa taarifa kuipeleka kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu tukio hilo kwa kuwa jambo hilo lipo chini yake.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkwamba, Juvenally Mmanzi alisema jana kuwa, ofisi yake ilipata malalamiko kutoka kwa mzazi wa mwanafunzi huyo.
Alisema walichukua jukumu la kwenda kumpima mtoto huyo katika Zahanati ya Mkwamba na kugundulika ni mjauzito wa miezi miwili na wiki moja.

“Baada ya kujiridhisha tulianza kumhoji binti huyo na kumtaka amtaje mhusika wa ujauzito huo, alimtaja mwalimu wake na kusema alikuwa katika mahusiano naye ya kimapenzi tangu akiwa darasa la tatu,” alisema Mmanzi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake