Baba Mzazi wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga akiwa anapokelewa Baada ya Kuwasili Dodoma Usiku huu
Mwili
wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga ukiwa unaingia nyumbani kwao Dodoma
Ukitokea Dar es salaam baada ya kutua Jana kutoka Marekani
Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga ukiwa umeshaingizwa ndani mwao usiku huu
Majonzi yakiwa yametawala nyumbani kwa wazazi wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga baada ya mwili kuwasili
Mama Zoe akiwa na majonzi baada ya kuwasili katika nyumba ya wazazi wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga
Mtumishi wa Mungu akiwa anafanya maombezi ya kushukuru kwa ndugu wote waliosafiri kufika salama
Ndugu jamaa na Marafiki wakiwa katika Msiba wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga usiku huu Dodoma
Picha zote na Fredy Njeje
Inasikitisha sana jamani,Mungu awatie nguvu wapendwa.
ReplyDeleteInasikitisha sana chozi limenitoka.
ReplyDeleteNaomba kuuliza ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unasema nini kuhusu kifo cha huyu kaka na wengine wote wanaouwawa.Sababu wako kimya sana na kwa kawaida naamini inabidi watuambie kitu, huyu ni mtanzania moja ya jukumu lao ni kufuatilia vitu kama hivi. Mmarekani akiuawa Tanzania unadhani watakaa kimya. Ingekua breaking news CNN.please watuambie inakuaje.
ReplyDeleteMsiombe ufiwe na mtoto.kuzika mtoto uliezaa mwenyewe maumivu hayaelezeki.Ni heri mtoto kuzika Mzazi ila Mzazi kuzika mtoto ni maumivu yasiyoisha.Hii habari hata usingizi sipati
ReplyDelete