Advertisements

Friday, May 20, 2016

NEYO APOKELEWA KAMA MFALME JIJINI MWANZA

Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka Festival 2016
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music' katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.

Msanii wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya Mwanza.
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake wakielekea jijini Mwanza leo jioni.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (t-shirt ya blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakijianda kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la Ndege la Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na 'crew' iliyoambatana na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakipanda ndani ya ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 mara baada ya kutua jijini Mwanza. 
Baadhi ya wapiga vyombo waliombatana na msanii wa Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa jijini Mwanza jioni. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (wa pili kushoto) na Mwanakamati ya Jembeka Festival 2016, Sharon wakiwasili na katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii. 
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla, Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika picha ya pamoja. 
Balozi wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza leo jioni.
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo aki-'show love' na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement aliyefika uwanjani hapo kumlaki na kumvisha shuka la Kimasai. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 
Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora Cultural Troupe cha jijini Mwanza akimshikisha nyoka aina chatu msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.

Waandishi wa habari wa jijini Mwanza wakiwemo wa JEMBE FM wakifanya mahojiano na msanii Neyo alipowasili jijini Mwanza.
Wakazi wa jijini Mwanza wakisalimana na msanii Neyo kwa shangwe na furaha waliofika kumlaki katika uwanja wandege wa jijini Mwanza.


Msafara wa msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo ukielekea hotelini baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Msanii Neyo alipowasili kwenye hoteli ya Malaika Resorts ya jijini Mwanza akiwapungia wafanyakazi pamoja na wateja katika hoteli hiyo.
Mwanasheria wa Jembe Media Group, Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa kutumbuiza kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

No comments: