ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 14, 2016

NYTC TANGAZO LA UCHAGUZI.

NYTC

TANGAZO LA UCHAGUZI.
Uchaguzi wa Viongozi wapya wa NYTC kwa kipindi cha tatu: May 14th, 2016 .
Kamati ya kujitegemea ya Uchaguzi wa viongozi wa NYTC kipindi cha tatu inawatangazia wanajumuiya wote kwamba kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wapya wa awamu ya tatu siku ya Jumamosi tarehe 14 May 2016, kuanzia saa saba mchana kwenye anwani ifuatayo:. 

30 Overhill Rd, 
Mt Vernon, NY 10552.

Ili uweze kupiga kura, unatakiwa uwe mwanachama hai kwa kulipa ada kufuatana na Katiba ya NYTC. unaweza kulipa dola 25 kwa miezi mitatu, dola 50 kwa miezi sita na dola 100 kwa mwaka mmoja. Kwa wanachama (walioishalipia ada zao) mnaombwa kuonyesha risiti zenu mlizofanyia malipo kabla ya kupiga kura.

Kufika kwenu kwa wingi na kupiga kura kuwapata viongozi wapya ndiyo mafanikio ya NYTC awamu ya tatu. Kupiga kura ni haki ya kila mwanajumuiya hai.
Ndg mwanajumuia akikisha upotezi haki yako.

KWANYONGEZA:
Katika siku hii muhimu ya uchaguzi NYTC, wanajumuhia wote mnakaribishwa kujumuika na familia zenu pamoja.
Kutakuwa na muziki, nyamachoma, vitafunwa, n.k pamoja na vinywaji baridi.

OMBI:
Tunaomba Mwajumuhia atakaejisikia kuleta chochote km chakula, vinywaji baridi nk , anakaribishwa kufanya hivyo.

MGENI WA HESHIMA:
Mhs Balozi
T. Manongi

MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI AWAMU YA TATU.

No comments: