Sunday, May 8, 2016

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA LUCY KIBAKI NCHINI KENYA.

Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.
Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.
Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

Imeandaliwa na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake