Mkuu wa mkoa wa Iringa akichangia mada
Mkuu wa Wilaya Iringa Mhe. Kasesela akichangia mada
Mkuu wa wilaya Iringa, Mkuu wa mkoa Iringa, Spika mstaafu bi Ana Makinda na Mkuu wawilaya ya Mfundi wakisikiliza mada
Mkuregenzi Mtendaji wa SAGCOT akitoa mada
Wadau wakisikiliza
Mkuu wa wilaya Ludewa Anatory Choya
Picha ya pamoja.
Pia Bi Neema Mwingu kutoka World Bank alitoa mada yenye kuonyesha kuwa Benki ya Dunia imetenga kiasi cha dola za kimarekani Milion 70 kukuza sekta binafsi inayokua (SME) ili waweze kushirikiana na wewekezaji wakubwa katika mnyororo wa thamani.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Njombe akiwakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bwana Anatoly Chonya alisema Mikoa ya Njombe na Iringa ndio mikoa ambayo ikifanya vizuri katika kilimo na ufugaji basi tanzania itakuwa imeongeza pato la taifa maradufu, aliwaomba SAGCOT kuhakikisha wanazidisha juhudi za kukuza kilimo katika mikoa hiyo. Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa bi Amina Masenza alisistiza suala la sekta binafsi kuhemshimu makubaliano ya awali hasa ya kunufaisha wanannchi walio wakuta, pia alichukizwa na mtindo wa makampuni hayo kuhamisha ulipaji wa kodi ya mapato kwenda Dar es salaam jambo ambalo linapunguza pato la mkoa kwa kiwango kikubwa. Naye Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bwana Jolwika Kasunga akichangia alisema " wawekezaji wana kuwa karibu sana na serikali mwanzoni wakati wa kuhangaikia vibali wanapo fanikiwa wanapotea mpaka wapate shida ingine" .
Naye Mkuu wawilaya ya Iringa Richard Kasesela alisistiza suala la masoko na wawekezaji kupata social licence kutoka katika jamii kabla ya kuanza uwekezaji hili litapunguza sana migogoro isiyo kuwa ya lazima. Katika mkutano huo pia Mkurugenzi wa Sagcot Catalyst Fund alisema lazima sasa wakulima wadogo wawe matajiri la msingi ni kuhakikisha fedha zote hizi zinawanyanyua na kuwafanya matajiri.
No comments:
Post a Comment