Mratibu wa Jumuiko la Maliasi Tanzania (TNRM), Faustine Ninga akifafanua jambo wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa Jamii wa Maliasili lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam
Demetrius Kweka kutoka Engility, (wasimamizi na waendeshaji wa mradi wa PROTECT), akizungumzia hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo
Manufaa yanayotokana na hifadhi za taifa na vivutio vya
utalii hayatoshi tu kutumika kama nyenzo ya kupunguza vitendo vya ujangili na
uvamizi katika maeneo yaliyotengwa na serikali ikiwa hakutakuwa na
ushirikishwaji wa kutosha na wa moja kwa moja kwa wananchi wanaoishi maeneo
yanayozunguka rasilimali hizo.
Pamoja na mchango mkubwa wa utalii katika uchumi taifa na
kuwepo kwa manufaa kwa vijiji vinavyozunguka hifadhi za taifa na vitutio
vingine vya utalii, jamii bado imeshindwa kuzitambua faida hizo ili kushiriki
kikamilifu katika kupambana na ujangili na uvamizi holela wa maeneo hayo.
Je, jitihada zinazofanywa na serikali na wadau kutoa elimu
kwa jamii na kuibua fursa muhimu katika sekta hii zinatosha?
Ili kujibu swali hilo Jukwaa linalohusu masuala ya Usimamizi
Shirikishi wa jamii wa maliasili mnamo Mei 26, 2016 limewakutanisha wadau wa
mazingira, maliasili na utalii kujadili mambo muhimu yanayoweza kuchangia
katika kufungua milango ya fursa katika sekta ya wanayamapori.
Wadau wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo
Afisa Utalii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii, Wilfred Msemo akiwasilisha mada
Meneja Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Selous, akiwasilisha
mada wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa Jamii wa Maliasili
lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment