Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salome Makamba aliyetaka kujua utayari wa Serikali wa kuruhusu viwanda Wilaya ya Kahama kufanya kazi masaa 24 ili kufidia uzalishaji uliokuwa haufanyiki kipindi umeme unapokatika nyakati za mchana.
Mhe. Jafo amesema kuwa, Serikali haijota zuio lolote kwa mashine katika Halmshauri hizo na amefafanua kuwa changamoto iliyopo ni kwamba viwanda hivyo vimekuwa vikitumia umeme wa jenereta ambao hautoshelezi kuendesha mashine wakati wote, hivyo kupelekea kuwepo na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Amefafanua kuwa, Halmshauri imewasiliana na Meneja wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) Kahama na tayari tatizo hilo limeanza kushughulikia ili kupata umeme wa uhakika kutoka Gridi ya Taifa ambapo tayari kituo cha usamabazaji kimeanza kujengwa Kahama.
Ameongeza kuwa Halmashauri inahamasisha wawekezaji wa viwanda vidogo vya kukoboa mpunga, mahindi na mazao mengine ili kupanua wigo wa mapato kupitia ushuru wa huduma (Service Levy) na ajira kwa vijana.
"Hakuna sababu yoyote kwa Serikali kuzuia wawekezaji katika viwanda vidogo na vikubwa, azma ya Serikali ni kupanua uwekezaji wa viwanda kadri iwezekenavyo kwa kuzingatia fursa zilizopo, tunachofanya ni kuboresha mazingira yatakayosaidia uwekezaji huo kufanyika kwa faida ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa umeme wa uhakika unakuwepo.
No comments:
Post a Comment