Sunday, May 8, 2016

WABUNGE ,JAMES MBATIA NA JOSEPH SELASINI WATEMBELEA WAHANGA WA MAAFA YALIYOTOKANA NA MVUA ROMBO

Wabunge James Mbatia (Jimbo la Vunjo ) na Joseph Selasini wakiwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya alipofika kutembelea wahanga wa mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha maafa.
Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini (kulia) akijaribu kutoa maelezo namna ambavyo wakazi wa kijiji cha Manda juu wilyani humo walivyo pata maafa yaliyotokana na kunyesha kwa mvua kubwa Aprili 24 na 25 mwaka huu.

Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa pole kwa wakazi wa kijiji cha Manda juu wilayani alipokua akielekea kujionea namna ambavyo baadhi ya familia zilivyo athirika na mvua katika kjiji hicho na mtoto mmoja kupoteza maisha baada ya kifusi kuporomoka na kuangusha nyumba aliyokuwemo.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ,Joseph Selasini (kushoto) akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kupuyo wakielekea kuijionea athari ya mvua hizo.
Mbunge Mbatia akizungumza jambo mara baada ya kufika katika eneo lililokuwa na nyumba iliyobomoka baada ya kuporomokewa na kifusi na kusababisha kifo cha mtoto mmoja katika kijiji cha Manda juu wilayani Rombo.
Baadhi ya majirani wa familia iliyopoteza mtoto katika kijiji cha Manda wilayani Rombo baada ya nyumba aliyokuwemo mtoto kuporomokewa na kifusi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
Sehemu ya mabaki ya nyumba iliyoanguka.
Eneo la Shamba la Migomba kama linavyoonekana baada ya kifusi kuporomoka .
Mbunge wa Jimbo Rombo,Joseph Selasini akizungumza jambo wakati vongozi wakifika eneo hilo kujionea hali halisi.
Baadhi ya viongozi walioambatana na wabunge hao wakijaribu kupanda kwenda kujionea hali halisi ya athari zilizotokana na mvua hizo.
Watoto wakionekana wakiwa wamesimama kwa juu sehemu ambayo ni hatari kwa usalama wao hasa kutokana na maeneo mengi ya muinuko katika eneo hilo udongo kuanza kuporomoka.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa tahadhari kwa wananchi wanaoendelea kusihi katika maeneo hayo huku akiutaka uongozi wa kijiji ,kata na wilaya kuhakikisha hakuna familia inaendele kuishi maeneo hayo hadi pale mvua zitakapo koma.
Viongozi pamoja na wananchi katika eneo hilo wakifanya sala kabla ya kuondoka katika eneo hilo.
Viongozi waliofika katika kijiji hicho wakiondoka eneo la tukio.
Sehemu ya nyumba zilizo athirika hivi ndivyo ilivyoonekana. Na Dixon Busagaga 

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake