Siku ya Jumamosi iliyopita (tarehe 21-Mei-2016) idadi kubwa ya wanajumuiya ya Watanzania wanaoishi katika jiji la Houston, Texas na vitongoji vyake walikutana na Bw. Todd Tyler ambaye ni Lead Detective wa kesi ya mauaji ya mpendwa wao Andrew Sanga aliyeuawa kwa kupigwa risasi takribani wiki tatu zilizopita na watu wasiojulikana . Sababu kubwa ya mkutano huo uliosimamiwa na uongozi wa Jumuiya wakiongozwa na Rais wa THC Bw.Daudi Mayocha ilikuwa ni kutaka kujua hatua ambayo kesi hiyo limefikia na kama wanajumuiya wanaweza kutoa mchango wowote katika kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa\watuhumiwa wa mauaji hayo.
Kwa kifupi mpelelezi huyo Bw.Todd Tyler alisema bado wanaendelea na uchunguzi na hadi siku hiyo alipokutana na wanajumuiya walikuwa bado hawajamkamata mtu yoyote kuhusiana na mauaji kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha hadi sasa. Bw.Tyler aliomba ushirikiano wa mtu yoyote ambaye ana taarifa itakayopelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa/watuhumiwa. Pata picha za tukio hilo hapa chini.
|
Bwana Tyler akiwasili kwenye mkutano na kupokelewa na Rais wa THC Bw.Mayocha
|
|
Bwana Tyler akiwa na Bw.Mayocha na Katibu Mkuu wa THC Bw. Ndejembi
|
|
Rais wa THC akifafanua jambo kwa Bw.Tyler |
|
Bw.Tyler akipitia orodha ya maswali yaliyoandaliwa na wana Houston |
|
Sehemu ya wana Jumuiya |
|
Wanajumuiya wakimsikiliza Bw. Tyler
|
2 comments:
So watu wote hawa kwaajili ya kuambiwa uchunguzi unaendelea si mngempigia simu tuu au email
Houstonian Bongolanders, what's going there? I thought the alleged killer was in the company of a Houston Kenyan. Now it sounds like nobody really knows anything about the suspect(s). Shouldn't we now be talking about an active manhunt?
Post a Comment