Yanga imekabidhiwa taji lao la ubingwa wa VPL msimu wa 2015-16 baada ya kufanikiwa kulitetea taji hilo ambalo walilitwaa msimu uliopita. Yanga imepewa kombe hilo ikiwa na pointi 74 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kutoshana nguvu na Ndanda FC kwenye uwanja wa taifa.Ndanda walianza kupata goli kwa mkwaju wa penati Omary Mponda lakini bao hilo lilisawazishwa na Simon Msuva dakika chache baadaye. Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la pili na kuiweka mbele klabu yake lakini Salum Minely akachomoa bao hilo na kuilazimisha Yanga kwenda sare kwenye uwanja wa taifa ambao Ndanda ndiyo walikuwa wenyeji katika mchezo huo.
Wachezaji wanakuwa na ndoto nyingi sana na pia huhitaji kuzikamilisha pindi wangali wana nguvu za kucheza, Wachezaji wa zamani wa Mbeya City Paul Nonga na Deus David wakiwa na furaha baada ya klabu yao kutwaa ubingwa.
Yanga ni klabu sahihi ambayo wanasoka wengi hukamilisha ndoto zao za kubeba ubingwa.
Familia ya Kamusoko.
No comments:
Post a Comment