ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 7, 2016

ZAIDI YA TANI 4579 ZA SUKARI ZAKAMATWA ZIKIWA ZIMEFICHWA DAR

Zaidi ya tani 4,579 za sukari zimekamatwa jijini Dar es Salaam baada ya Rais Dkt John Magufuli kuviagiza vyombo vya dola kufanya msako wa kuwabaini wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa makusudi ili kupandisha bei ya bidhaa hiyo.
Kwa mujibu wa TBC One, taarifa ya Mkurugenzi wa Utafiti wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU, imebaini uwepo wa sukari iliyonunuliwa kutoka kiwanda cha sukari cha Kilombero na kufichwa katika maghala mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara huyo ameficha sukari hiyo Mbagala na Tabata na kuwafanya wafanyabiashara wa reja reja kuikosa.

No comments: