Advertisements

Thursday, May 26, 2016

ZSTC YAKABIDHI FIDIA KWA WANANCHI

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar, (ZSTC),Ndg.Maalimu Kassim Suleiman, akizungumza na Waathirika walioanguka Mikarafuu katika msimu wa zao hilo kisiwani Pemba kwa mwaka 2015/2016 wakati wa malipo ya fidia, hafla hiyo ya kukabidhi fidia kwa Wabnanchi hao imefanyika katika Ukumbi wa Makonyo Wawi Chakechake Pemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC), Ndg.Maalimu Kassim Suleiman,akimkabidhi fedha za fidia mmoja ya Mwananchi aliyeaguka Mkarafuu Kiwani Pemba wakati wa hafla ya kukabidi fedha hizo kwa wananchi waliopata ajali za kuanguka mkarafuu kisiwani Pemba hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa makonyo Wawi Chakechake Pemba.Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la ZSTC, Maalimu Kassim Suleiman,akizungumza na mtoto ambae alianguka Mkarafuu msimu wa 2015/2016.huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi.
Mtoto ambae alianguka Mkarafuu msimu uliopita akiweka saini baada ya kukabidhiwa fedha za Fidia kutoka mfuko wa maendeleo ya Karafuu huko Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu Zanzibar, Ndg.Ali Suleiman Mussa, akizungumza na waandishi wa habari kisiwani Pemba kuhusiana na Wananchi waliopata ajali ya kuanguka mkarafuu.(Picha na Bakar Mussa-Pemba.)

No comments: