Wednesday, June 8, 2016

Dr. KIGWANGALLA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA UKIMWI WA UMOJA WA MATAIFA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dr.Hamis Kigwangalla ( Mb) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Tanzania Dr. Hamis Mwinyimvua, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Policy &Coordination) na Mhe. Constantine Kanyasu ( Mbunge wa Geita na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi, katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa Mkutano wa ngani ya juu kuhusu Ukimwi ambao umeandaliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mkutano huyu umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon 

Na Mwandishi Maalum, New York

Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa, kuhusu masuala ya ugonjwa wa Ukimwi umeanza leo ( Jumatano) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu wa siku tatu na ambazo umeandaliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa Kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi ( UNAIDS),unaongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dr. Hamis A Kigwangalla (Mb).

Wengine katika ujumbe ni Dr. Hamis H. Mwinyimvua Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Policy & Coordination), Mhe. Constantine John Kinyasu. Mbunge wa Geita Mjini na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi, Dr. Fatma Mrisho Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS na wataalamu mbalimbali.

Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema kunahatua kubwa zimefikiwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi.

Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na ongeko la idadi ya watu wanapata huduma za dawa za kuzuia makali ya ukimwi. Ongezeko hilo kwa mijibu wa Katibu Mkuu limechangiwa na upatikanaji wa dawa za gharama nafuu.

“Mpaka leo hii, zaidi ya watu 17 milioni wanapatiwa huduma hiyo na hivyo kuokoa maisha ya mailioni ya watu na wakati huo huo kuokoa mabilioni ya fedha.

Mafanikio mengine yametajwa kuwa ni pamoja na kupungua wa maambukizo kwa asilimia 35 tangu mwaka 2000, kupungu kwa asilimia 43 ya vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa ukimwi tangu mwaka 2003.

“ Ninayofuraha kwamba maambukizi mpya ya virusi vinavyosababisha ukimwi kwa watoto yamepungua kwa asilimia 56 katika kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita. Ili hali nchi nne, cuba, Thailand, Armenia na Belarus hakuna kabisa maamkizo kwa watoto. Ni matumani yangu tutakifia mahali pakuwa na sifuri ya maambuki kwa watoto” akasisitiza Ban Ki Moon.

Pamoja na mafanikio hayo yote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametahadharisha kwamba kama jumuiya ya kimataifa haitatumia mafaniko hayo kuongeza kasi zaidi na kushughulikia tatizo la ukimwi kwa nguvu zaidi kunauwezekano mkubwa kwamba ugonjwa huo ukarudi kwa kasi kubwa zaidi kulivyo ilivyo sasa na hususani katika nchi zenye uchumi mdogo na wakati.

Viongozi wengine waliozungumza wakati wa ufunguzi ni pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw Monges Lykketoft na Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Michael Sidibe.Katika siku hii ya kwanza ya mkutano wa kilele kuhusu Ukimwi, wajumbe kutoka karibu mataifa yote duniani ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, walipitisha tamko la kisiasa kuhusu matokeo ya mkutano huu.

No comments: