Saturday, June 4, 2016

HATUJAMKATAA MH MASILINGI

Salma Moshi akisalimiana na Mhe. Balozi Wilson Masilingi siku ya misa ya mpendwa wetu marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, kushoto ni mume wa marehemu Madaraka Nyerere.

Mimi kama Mkazi wa siku nyingi hapa USA Marekani nimesikitishwa na niliyoyasikia bungeni kuwa tumesaini petition ya kumkataa Mh Balozi.

Mh Masilingi amekuwa Balozi kwa Miezi minane tu toka ateuliwa amefanya Mengi makubwa pamoja na kukutana na WaTanzania wa State Mbalimbali nakutusaidia nakutuelekeza na kutuwezesha kuwekeza Nyumbani kwa kwashirikiana na wawekezaji wa hapa pia ametusaidia sana ana uchungu wa Maendeleo na sisi WaTanzania tuishio America.

kuhusu misiba ameshiriki misiba mingi tu toka aingie hapa takrbani miezi 8
misiba iliyotokea Huston Alituma Mwakilishi kutoka Ubalozini na pesa kwa familia zote kama pole kwa wafiwa kwani siku hiyo hakuwa kwenye party kama ilivyoelezwa Bungeni alikuwa anamwakilisha Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwenye kongamano  la DICOTA na kusoma hotuba salam kutoka kwa Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

lakini kama kuna vifo kama hivyo vipo vilivyotokea hapa
kijana Mwanafunzi wa Howard University alipigwa risasi umri mdogo miaka 22 mbona hakuongea OMARY SYKES

Kuna mtoto wa Capt Mazula Rubani maarufu Tanzania Alikuwa Mwanafunzi yeye na girlfriend wake Wote WaTanzania Waliuwawa na wakachomwa moto mbona hajasema
Asipotoshe Umma Mnaoingia Bungeni na Wananchi muelewe

mimj Salma Mkazi wa USA zaidi ya miaka 10 sijaona Bendera kuchanika iko kipande kama alivyoongelewa Bungeni.

Ni mimi Salma Moshi mkaazi wa DMV

7 comments:

Anonymous said...

Asante saana dada salma. Mimi mwenyewe ninafurahia ushirikiano wake na jamii ya watanzania hapa USA. Lakini ikumbukwe kwamba mh masilingi hakuja marekani kuhani misiba au vivyo vya watanzania. Alikuja kwa shugh'uli za kiserikali.hata ukisikiliza hotuba zake,utajua kuwa anapenda watu. Ninahisi tumetawaliwa na wivu na majungu. Ningemuomba kuitisha mkutano na watanzania Waishio Washington DC na kila mmoja amweleze matatizo yake. Vilevile ikumbukwe mh, masilingi si kazi yake kwenda kila state kuhani misiba. Kuna kikundi cha watu wachache wenye itikadi zao za vyama,dini na ukabila ndivyo vinavyochangia matatizo yetu.wengine wanajifanya marafiki wa karibu saana. Ogopa watu wanamna hii. Vilevile nitamshangaa mh,Rais pamoja na mh,masilingi kusikiliza ujinga huu. Na nivizuri hawa watu wakajulikana kwani ni vidonda ndugu.

Anonymous said...

Funguka zaidi, nini kiliongelewa bungeni na nani aliyewakilisha agenda hiyo, kwani si wote tuna access ya kupata taarifa za kila linaloendelea bungeni.

Anonymous said...

Safii tunapampenda.Balozi wetu.

Anonymous said...

Huyo mbunge ni nani na kapata wapi hizo habari za petition? Mimi ni mwanajumuia ya DMV lakini sifahamu uwepo wa petition kama hiyo. Au petition hiyo ni ya watu fulani fulani tu? Wabongo tuacheni majungu, hayajengi!

Anonymous said...

Salma acha kujipendekeza,ukutumwa,Kuna sababu ya wenzio kulalamika,acha tabia yako ya kuwa kimbelembele kama ujaolewa,wacha ukweli ijulikane tu.

Anonymous said...

Jamani huyo aliyesema tumkemkataa nani

Anonymous said...

Hao walioandika walaka wa kumtuhumu Mheshimiwa balozi Masilingi wana ajenda Yao ya Siri ya kutaka kumchafua , kwa maoni yangu Mimi nadhani wanatumiwa na wanasiasa, hawa watu ni wa kupuuzwa tu. Balozi hahitaji kuitisha kikao kwa watanzania wanaoishi DMV kuwauliza / kuwasikiliza matatizo yao kwa sababu ya wapuuzi fulani eti kwa sababu wametoa walaka wa kumtuhumu Balozi kwa sababu ambazo si za kweli, Watanzania tuacheni majungu jamani, watu mnaishi dunia ya kwanza lakii hambadiriki loh!! Mnajifedhehesha sana!!